Rais wa zamani wa Afrika Kusini
Thabo Mbeki amewasili mjini Khartoum katika jitihada za kufufua
mazungumzo kati ya Sudan na jirani zao Sudan kusini.

Mpatanishi Thabo Mbeki awasili Sudan
Shirika la Umoja wa Mataifa limetishia kuziwekea nchi hizo mbili vikwazo.
Kulingana na kamati ya usalama ya Umoja wa Mataifa , nchi hizo mbili zilipaswa kuanza gumzo kati yao wiki iliyopita.
Sudan kusini kwa upande wake inasema iko tayari kurudi katika meza ya mazungumzo bila ya masharti yeyote. Lakini Sudan kwa upande wake inasisitiza kuwa gumzo kati yao lazima lijikite katika swala la usalama.

No comments:
Post a Comment