Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
amekutana na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa, Anna
Tibaijuka na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya
Huvisa, kwa mazungumzo na kupokea taarifa ya zoezi la bomoa bomoa nyumba
zilizojengwa maeneo ua ufukweni, ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni.
Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Dar es Salaam jana Mei 17, 2012. Katika picha kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi,
Veldiana Mashingia, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka (kulia), Mkurugenzi wa Mazingira, Dk. Julius Ningu na Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Dk. Terezya Huvisa, baada ya
mazungumzo hayo. (Picha zote na Muhidin Sufiani-OMR )
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal,
akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Profesa Anna
Tibaijuka (kushoto) na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Terezya
Huvisa (wa pili kulia), mara baada ya mazungumzo yao kuhusu zoezi la ubomoaji wa nyumba
zilizojengwa maeneo ua ufukweni, ambalo linatarajia kuanza hivi karibuni.
Mazungumzo hayo yalifanyika ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu Dar es Salaam jana
Mei 17, 2012. Kulia ni Mkurugenzi wa Mazingira,
Dk. Julius Ningu.



No comments:
Post a Comment