TANGAZO


Tuesday, May 22, 2012

Airtel yasaini mkataba wa Airtel Rising Stars na DRFA


Afisa Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jane Matinde (kulia), akitilia saini mkataba wa kudhamini michuano ya vijana wenye umri ya miaka 17 ya Airtel Rising Stars 2012, huku mjumbe wa Kamati ya mashindano hayo mkoani Dar es Salaam, Daudi Kanuti akishuhudia. Wengine ni Katibu Mkuu wa TFF, Angetile Osiah (aliyesimama kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano TFF, Saad Kawemba. Hafla hiyo ilifanyika jana Mei 21 kwenye ofisi za TFF.

Mjumbe wa Kamati ya Mashindano Dar es Salaam, Daudi Kanuti naye akitia saini mkataba huo.

Afisa Uhusiano Airtel Tanzania, Jane Matinde, akikabidhi mkataba wa kudhamini michuano ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 kwa mjumbe wa kamati ya mashindano ya Dar es Salaam, Daudi Kanuti baada ya kutia saini udhamini huo. Wengine ni Katibu Mkuu wa TFF Angetile Osiah (wa pili kushoto) na Mwenyekiti wa Kamati ya mashindano TFF, Saad Kawemba. Hafla hiyo ilifanyika jana Mei 21, Ofisi za TFF jijini.

No comments:

Post a Comment