Erik Magesa wa Toto Africa, akimtoka Felix Sunzu wa Simba.
Fabian Ngwase wa Toto Africa ya Mwanza (nyuma), akipambana na Salum Machaku wa Simba katika mchezo huo.
Salum Machaku wa Simba, akijaribu kuudhibiti mpira huku akizongwa na Ladislaus Boniface wa Toto Africa.Emmanuel Okwi wa Simba, akimtoka Idd Mobby wa Toto Africa katika mchezo huo.
Haruna Moshi 'Boban', akiudhibiti mpira mbele ya Erik Magesa (kulia) na Mussa Mussa wa Toto Africa, wakati timu hizo zilipopambana katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam leo.
Haruna Moshi wa Simba (katikati), akiudhibiti mpira huku akifuatwa kwa karibu na Mussa Mussa (kulia) na Erik Magesa wa Toto Africa, wakati wa mchezo huo.
Mashabiki wa Simba wakifuatilia kwa makini mchezo kati ya timu yao na Toto Africa ya Mwanza, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam leo Machi 11, 2012.







No comments:
Post a Comment