TANGAZO


Monday, February 27, 2012

OTTU Band yavamia ukumbi wa Max Bar, Ilala Bungoni

 Waimbaji wa Msondo Band, kutoka kushoto, Edo Sanga, Shaaban Dede na Juma Katundu, wakiimba wimbo mpya wa bendi hiyo, unaoitwa Nadhiri ya Mapenzi wakati kundi hilo, lilipotumbuiza, ukumbi wa Max Bar, Ilala Bungoni, Dar es Salaam juzi. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Mwimbaji mkongwe wa kundi hilo, Muhidini Gurumo, akiimba wimbo unaoitwa Faulata, wakati kundi hilo lilipotumbuiza ukumbi wa Max Bar, Ilala Dar es Salaam jana.


 Mwimbaji Hassan Moshi, akitunzwa pesa na shabiki wa kundi hilo, wakati hilo, lipotumbuiza kwenye ukumbi huo jana.


 Wapiga midomo Roman Mngande (kulia) na Hamis Mnyupe wakirapu wakati wa onesho hilo, ukumbini hapo jana. (Picha na Kassim Mbarouk)


 Waimbaji Edo Sanga (kushoto), Shaaban Dede (kulia), wakionesha ufundi wao wa kuimba katika onesho hilo, ukumbini humo juzi.


Roman Mngande (kushoto) na Shaaban Dede, wakimba huku wakizirudi ngoma za kundi hilo, baada ya kuchenguliwa na gitaa la Solo, lililokuwa likiungurumishwa na Abdul Ridhwan katika onesho hilo, ukumbi wa Max Bar, Ilala Bungoni, Dar es Salaam juzi.


 Mnenguaji wa OTTU Banda, Queen Vero, akizirudi ngoma za kundi hilo, wakati lilipotumbuiza Ukumbi wa Max Bar, Ilala Dar es Salaam juzi.


 Mnenguaji Amri Saidi 'Super Dongo', akizirudi ngoma za kundi hilo wakati wa onesho hilo juzi.


 Mnenguaji Khadija Mapozi, akionesha ufundi wa kunengua wakati wa onesho hilo, juzi usiku ukumbini humo.



Mashabiki wa kundi hilo, wakizirudi ngoma hizo wakati wa onesho hilo, ukumbini humo.

No comments:

Post a Comment