Mfanyabiashara wa Malaysia, Money Tou (kulia), akiwapatia maelezo wananchi waliofika kwenye banda la Kampuni ya Fubisun Trading, kwenye maonesho ya Kimataifa ya Syria, yanayofanyika nchini, ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam leo. (Picha na Kassim Mbarouk)
Mfanyabiashara wa Syria Saed Bassam, akiwapaka mafuta mazuri, wananchi waliofika kwenye banda lao la Kampuni ya Lawssan kwenye maonesho hayo.
Wananchi wakiangalia mashuka ya kutandika kitandani yaliyokuwa yanaoneshwa kwenye maonesho hayo ya wafanyabiashara wa Syria nchini.
Rahma Shaaban, akiwapatia maelezo wananchi waliofika kwenye banda la Kampuni ya Ziad, inayojishughulisha na bidhaa za mafuta, sabuni na vipodozi vya ngozi na nywele kwenye maonesho hayo.
Baadhi ya bidhaa zinazooneshwa kwenye maonesho hayo, zikiwa zimetungikwa kwenye moja ya mabanda ya Kampuni zinazoshiriki kwenye maonesho hayo. Hapa yanaonekana majambia (chini) na panga (juu), huku kijana (kushoto), akiwa tayari kwa ajili ya kutoa maelezo na pia kuuza bidhaa hizo kwa wananchi wanaozihitaji.






No comments:
Post a Comment