TANGAZO


Wednesday, February 29, 2012

Makamu wa Rais, Dk. Bilal, amaliza ziara ya Iringa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wanafunzi wa shule ya Sekondari ya Iwawa baada ya kuzungumza nao wakati akimaliza ziara yake ya Wilaya ya Makete, mkoani Iringa jana,  Februari 28, 2012. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na wananchi pamoja na wanafunzi wa Shule hiyo, baada ya kuzungumza nao wakati akimaliza ziara wilayani Makete, Mkoa wa Iringa, jana Februari 28, 2012.


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi cheti cha kumiliki hisa za Benki ya Wananchi (NJOCBA), Olive Luena, bada ya kuizindua rasmi benki hiyo, iliyopo Wilaya ya Njombe, mkoani Iringa jana.


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akifurahia jambo na Mwenyekiti wa Bodi wa benki ya Wananchi ya (NJOCOBA), Twilumba Ulaya, baada ya kuizindua benki hiyo jana. 


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mkurugenzi wa Nishati wa kiwanda cha Sao Hill, Roselyne Mariki, wakati alipowasili katika kiwanda hicho jana kwa ajili ya kuzindua mashine mpya na ya kisasa ya kuchana mbao.

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akimsikiliza Mkurugenzi Mkuu wa kiwanda cha mbao cha Sao Hill, Nick Moore, kuhusu ufanyaji kazi wa mashine mpya ya kisasa ya kuchana mbao iliyoizindua katika kiwanda hicho jana, wakati alipokuwa akimaliza ziara yake ya Mkoa wa Iringa. 


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya wafanyakazi wa kiwanda cha Sao Hill, Erlend Haugen, ambaye ni mrefu kuliko wafanyakazi wote wa kiwanda hicho, baada ya kuizindua mashine ya kuchania mbao katika kiwanda hicho jana. 

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya silaha ya jadi ya kabila la Wahehe (mkuki), kutoka kwa mjukuu wa Chifu Mkwawa, Ignas Muyinga, baada ya kumaliza kuzindua kituo cha afya na kuwahutubia wananchi wa kijiji cha Lungemba, Wilaya ya Mafinga mkoani Iringa jana. 

No comments:

Post a Comment