Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akielekezwa na mtafiti bingwa duniani wa sokwe, Jane Goodall, kuhusu ishara anazozitumia kuwasiliana na sokwe na
jinsi ya kuzungumza nao, wakati alipofika Ikuu ndogo ya Wilaya ya Mpanda, Mkoa wa
Katavi leo. (Picha na Muhidin Sufiani PMO)
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akielekezwa na mtafiti
bingwa duniani wa sokwe, Jane Goodall, kuhusu ishara anazozitumia
kuwasiliana na sokwe na jinsi ya kuzungumza nao.
Makamu wa Rais, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipokea zawadi ya kitabu
cha mtafiti bingwa duniani wa sokwe, Jane Goodall, aliyefika
Ikulu ndogo ya Wilaya ya Mpanda mkoa wa Katavi leo kwa ajili ya
mazungumzo. Jane amekaa nchini kwa miaka 50 akifanya utafiti
katika mapori ya Gombe na Mahale yaliyopo mkoa wa Kigoma na
Katavi.
Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Asha Bilal,
wakizungumza na mtafiti bingwa wa sokwe duniani, aliyekaa nchini
kwa miaka 50 akifanya utafiti wa Masokwe katika mapori ya Gombe
na Mahale, Jane Goodall, wakati alipofika Ikulu ndogo Wilaya ya
Mpanda mkoa wa Katavi kwa ajili ya mazungumzo leo.
Makamu wa Rais Dk. Gharib Mohammed Bilal, akiwa katika picha ya pamoja
baada ya mazungumzo.
No comments:
Post a Comment