TANGAZO


Tuesday, February 21, 2012

Waziri Nchimbi awapatanisha Ruge na Mr II

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaa leo, kuhusu upatanishi na kumalizika kwa mgogoro wa miaka miwili uliotokana na sababu za kimuziki baina ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi (Katikati) na Mkurugenzi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba (kulia). Wapatanishi wa mgogoro huo, ni  Waziri Dk. Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu. (Picha na Anna Itenda - Maelezo)




Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kumalizika kwa uhasma kati yao na  Mkurugenzi wa Clouds Media,  Rugem Mutahaba (kulia), uliomalizwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lisu (hawapo pichani), Dar es Salaam leo.




 
Mkurugenzi wa Clouds Media, Ruge Mutahaba, akizungmza na waandishi wa habari wakati wa kuelezea kuhusu upatanishi huo.  Kushoto ni aliyekuwa mgomvi wake, Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi.



Mbunge wa Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media Ruge Mutahaba, wakipeana mikono, Dar es Salaam leo, ikiwa ni ishara ya kupatana na kumaliza kwa tofauti zao zilizotokana na sababu za kimuziki zilizodumu kwa muda wa miaka miwili. Kushoto ni Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dk. Emmanuel Nchimbi na kulia ni Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lisu waliopatanisha mgogoro huo.

No comments:

Post a Comment