Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi
na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato cha sita, Burilo
Busagi, katika mahafali ya kidato cha sita shule ya Sekondari Nsumba, jijini Mwanza leo.
Jumla ya wahitimu 374 wa kidato hicho walipewa vyeti. Kushoto ni Mkuu wa shule
hiyo Josephat Zakeyo.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akimkabidhi cheti mhitimu wa kidato
cha sita, Tifugundulwa Tumbika katika mahafali ya kidato cha sita shule ya
Sekondari Nsumba, Mwanza. Tumbika alikabidhiwa cheti hicho kwa kuibuka
mwanafunzi bora katika kuzungumza Kiingereza. Wapili kulia ni Mkuu wa shule hiyo
Josephat Zakeo.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya
Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na mwanafunzi aliyesoma
shule ya sekondari ya Nsumba, Mwanza, kati ya mwaka 1954 na 1957 (darasa la nane
na kumi) Damas Ngoma, wakati wa mahafali ya kidato cha sita ya shule hiyo leo.
Nape ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo alisoma pia katika shule
hiyo hadi kidato cha nne mwaka ambako alimaliza mwaka 97. Watatu ni Mkuu wa
shule hiyo Josephat Zakeo.(Picha na Bashir Nkoromo).
No comments:
Post a Comment