TANGAZO


Thursday, January 19, 2012

Makamu wa Rais aifariji familia ya marehemu Jeremiah Sumari


 


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na watoto wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Masharikina, Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu, Tang Bovu jijini Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa. (Picha na Muhidin Sufiani-OM)


Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akiweka saini katika kitabu cha maombolezo ya aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremia Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu, Tangi Bovu jijini leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole  kwa wafiwa, kufuatia kifo cha mbunge huyo.
Makamu wa Rais Dk. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na mke wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremiah Sumari, Mama Miriam Sumari, wakati alipofika nyumbani kwa marehemu Tang Bovu kuwafariji wafiwa kufuatia kifo cha mbunge huyo, kilichotokea usiku wa kuamkia leo, Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alikokuwa amelazwa. (Picha na Muhidin Sufiani-OMR)

Makamu wa Rais, Dk. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na mke wa aliyekuwa Mbunge wa Arumeru Mashariki na Naibu Waziri wa Fedha, marehemu Jeremiah Sumari, Mama Miriam Sumari, wakati alipofika nyumbani kwao, Tangi Bovu, Dar es Salaam leo Januari 19, 2012, kwa ajili ya kutoa pole kufuatia kifo cha mbunge huyo kilichotokea usiku wa kuamkia leo Hospitali ya Taifa Muhimbili alikokuwa amelazwa.

No comments:

Post a Comment