TANGAZO


Sunday, August 27, 2017

MAHAFALI YA 10 YA SHULE YA SEKONDARI YA WASICHANA YA JOHN BAPTIST BOKO BASIHAYA JIJINI DAR ES SALAAM YAFANA

Wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist ya Boko Basihaya, jijini Dar es Salaam, wakiongozwa na bendi maalum katika gwaride la kuingia katika viwanja vya shule hiyo, wakati wa mahafali yao ya 10 ya shule hiyo, jijini jana. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Wahitimu wa kidato cha nne wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist ya Boko Basihaya, jijini Dar es Salaam, wakiingia katika viwanja vya shule hiyo, wakati wa mahafali yao ya 10 ya shule hiyo, jijini jana.  
Mgeni Rasmi katika mahafali hayo, Profesa Lucian Msambichaka (kulia), akiwa na baadhi ya wakuu wa shule hiyo katika mahafali hayo. 
Mgeni Rasmi katika mahafali hayo, Profesa Lucian Msambichaka (wa tatu kulia), akiwa na baadhi ya viongozi na wakuu wa shule hiyo katika mahafali hayo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo, John Mayanja na wa pili ni Mkurugenzi wa shule, Jalia Mayanja.
Baadhi ya wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili wa shule hiyo, wakiwa katika mahafali hayo. 
Wahitimu wa kidato cha nne wakiwa katika viwanja vya mahafali hayo, shuleni hapo, jijini jana.  
Wahitimu wa kidato cha nne wakiimba moja ya nyimbo zao, wakati wakiaga katika mahafali hayo, shuleni hapo, jijini jana.

Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist ya Boko jijini Dar es Salaam, Jalia Mayanja (kushoto), akielezea kuhusu slogan ya 3D ya shule hiyo, wakati wa uzinduzi katika Mahafali ya 10 ya Kidato cha Nne yaliofanyika shuleni hapo jana. Wa kwanza kulia ni Mgeni rasmi wa mahafali hayo, Profesa Lucian Msambichaka.
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist ya Boko jijini Dar es Salaam, Jalia Mayanja (kushoto), akicheza ngoma ya msanii Saida Karoli, sambamba na wanafunzi wa shule hiyo, wakati wa mahafali ya 10 ya kidato cha nne yaliyofanyika jana shuleni hapo.

Wanafunzi wa kidato cha kwanza na cha pili wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist ya Boko jijini Dar es Salaam, akicheza ngoma ya msanii Saida Karoli, wakati wa mahafali hayo shuleni hapo jana.
Mhitimu wa kidato cha nne, Dorothy Boke, akisoma risala ya wahitimu wakati wa mahafali hayo, shuleni hapo, jana. 
Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist ya jijini Dar es Salaam, Jalia Mayanja akitoa hotuba yake, wakati wa mahafali hayo.

Mkurugenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist ya jijini Dar es Salaam, Jalia Mayanja akitoa hotuba yake, wakati wa mahafali hayo.

Mgeni rasmi wa mahafali hayo, Profesa Lucian Msambichaka, akitoa hotuba yake.

Mwanafunzi Bora wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist ya Boko jijini Dar es Salaam, Lilian Madole, akikabidhiwa cheti maalum na Mgeni rasmi wa Mahafali ya 10 ya shule hiyo, Profesa Lucian Msambichaka jijini jana.
Rais wa wanafunzi, Dorothy Boke, akitunukiwa cheti na mgeni rasmi katika mahafali hayo, Profesa Lucian Msambichaka kutokana na Uongozi Bora aliouonesha katika uongozi wake. 
Mmoja wa wahitimu wa kidato cha nne akitunukiwa cheti cha kuhitimu katika mahafali hayo na mgeni rasmi, Profesa Lucian Msambichaka. 
Mgeni rasmi katika mahafali hayo, Profesa Lucian Msambichaka akimtunuku Waziri Mkuu wa Serikali ya wanafunzi, Victoria Muhandiki cheti kutokana na uongozi wake.

Na Mwandishi Wetu
WALIMU, Wanafunzi na Wafanyakazi katika shule mbalimbali wametakiwa kuzingatia nidhamu shuleni ili kuweza kuchochea maendeleo ya ufaulu kwenye shule zao.


Wito ulitolewa jana na Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya John Baptist iliyopo Boko Basihaya jijini Dar es Salaam, Aspiter Kibona wakati wa mahafali ya 10 ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyoenda sambamba na uzinduzi wa kampeni ya '3D' yenye maana ya !Nidhamu, Nidhamu, Nidhamu!.


Kibona alisema wameamua kuzindua kampeni hiyo ikiwa ni kauli mbio yao kwa wanafunzi wa shule hiyo pamoja na walimu na wafanyakazi wengine kuzingatia nidhamu muda wote ambayo itaendelea kuchochea maendeleo ya ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.


"Nidhamu si kwa wanafunzi pekee bali inatakiwa kuanzia hata kwangu mimi mkuu wa shule pamoja na walimu na wafanyakazi wengine katika shule yetu hii, hivyo tumezindua kampeni hii ikiwa ni kauli mbio yetu ya kuendelea kuhamasisha nidhamu katika shule yetu kwa nia kuendelea kuchochea maendeleo ya wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao darasani, " alisema Kibona.


Alisema nidhamu inapoanzia kwa viongozi wa juu, walimu na wafanyakazi wengine inasaidia nidhamu hiyo hiyo kuingia hadi kwa wanafunzi ambayo inawachochea kufanya vizuri katika masomo yao darasani.


Naye Mkurugenzi wa shule hiyo, Jalia Mayanja aliwataka wahimu 53 wa kidato cha nne kuzingatia nidhamu mahali popote watakapokuwa mara baada ya kutoka shuleni hapo kwa faida yao ya huko waendako.


Mayanja alisema nidhamu ndiyo siri ya mafanikio ya shule hiyo katika ufaulu kwa wanafunzi wa shule hiyo.
Alisema ni vema wahitimu hao wa kidato cha nne wakaendeleza nidhamu waliyokuwa wakiionyesha shuleni hapo huko wanapokwenda ili iweze kuwasaidia katika maisha yao ya baadae.


Aliongeza kwa kuwataka wazazi wanaopeleka watoto wao katika shule hiyo kukaa kwa amani kutokana na kwamba wapo katika mikono salama.

No comments:

Post a Comment