Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisalimiana na baadhi ya viongozi wa Jeshi la Magereza na Mfuko wa pensheni wa PPF baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro kwa ajili ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi pamoja na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kipya eneo la Karanga Moshi Mkoani Kilimajaro.
Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro Anna Mghwira alipofika katika eneo la mradi wa ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi kilichopo Karanga Moshi Mkoani Kilimajaro kinachoendeshwa kwa ushirikiano kati ya PPF na Jeshi la Magereza.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango wakiangalia moja ya jozi ya kiatu kilichotegenezwa na kiwanda cha Karanga ambacho kinafanyiwa marekebisho ili kuongeza uzalishaji, Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama (wa pili kutoka kushoto), Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango (watatu kutoka kushoto), Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda na Mkuu (wakwanza kutoka kushoto), Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni (wa nne kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro Mama Anna Mghwira wakiangalia moja ya jozi ya kiatu kilichotegenezwa na kiwanda cha Karanga Kilichopo mkoani Kilimanjaro kinachoendeshwa kwa ushirikiano kati ya PPF na Jeshi la Magereza.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni za wastaafu PPF, Bw.William Erio akitolea maelezo kuhusu mipango ya ujenzi wa kiwanda kipya cha bidhaa za ngozi ambapo alisema kiwanda hicho kitagharimu bilioni 54.4 na kitakuwa na uwezo kuzalisha futi mraba za ngozi milioni tatu laki saba na nusu kwa mwaka pamoja na kuzalisha viatu vya kijeshi na kiraia jozi milioni moja na laki mbili kwa mwaka, pamoja na kutoa soli laki tisa kwa mwaka pamoja na kutoa bidhaa nyingine za ngozi kama mikanda,mabegi na mikoba ya akina mama takribani elfu arobaini na nane kwa mwaka.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akipimwa mguu ili kutegenezewa kiatu alipofanya ziara katika eneo la mradi wa uboreshaji na ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi cha Karanga Moshi Mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango, Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji Prof. Adolf Mkenda na Mkuu, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni, na Mkuu wa Mkoa wa Kilimajaro Mama Anna Mghwira wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa PPF na Jeshi la Magereza baada ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi pamoja na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kipya eneo la Karanga Moshi Mkoani Kilimajaro.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akiongea baada ya ziara ya ya kutembelea kiwanda cha kuzalisha bidhaa za ngozi pamoja na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa kiwanda kipya eneo la Karanga Moshi Mkoani Kilimajaro ambapo aliipongeza PPF pamoja na Jeshi la Magereza kwakufanya maamuzi sahihi yanayoendana na dira ya Serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda kwa kuja na mradi wa uboreshaji na ujenzi wa kiwanda kipya cha kuzalisha bidhaa za ngozi cha Karanga Moshi Mkoani Kilimanjaro. (Picha zote na Maelezo)
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge, Ajira na Watu wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama ameipongeza bodi ya wadhamini ya Mfuko wa Pensheni wa PPF kwa uamuzi wa kushirikiana na Jeshi la Magereza katika kujenga kiwanda kipya pamoja na kuendeleza kiwanda cha Bidhaa za ngozi Karanga Kilichopo Mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea na kuona maendeleo ya kiwanda hicho Waziri Mhagama amesema kuwa PPF na Jeshi la Magereza wamefanya maamuzi sahihi yanayoendana na dira ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda.
“Dhamira ya Serikali ni kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda, PPF na Jeshi la Magereza mmeonesha mfano, uboreshaji wa kiwanda hiki na ujenzi wa kiwanda kingine ambacho kitakuwa na viwanda vidogovidogo vinne ni ishara ya kutimia kwa ahadi ya Rais wetu Dkt. John Magufuli ya kuwa na uchumi wa kati kupitia Viwanda”. Alisema Mhe. Jenista.
Aidha, alisema kuwa lengo la Serikali ni kuhakikisha mradi huu unatekelezwa kwa kiwango cha kuridhisha na Serikali itatoa msaada popote inapohitajika ili kwa haraka nchi yetu ianze kuzalisha viatu ambavyo vitauzwa nje ndani na nje ya nchi hatimaye kuliingizia taifa mapato.
Akizungumzia kuhusu ajira zitakazozalishwa na kiwanda hicho Waziri Mhagama amesema kuwa kiwanda hiki pekee kitatoa ajira za moja kwa moja 689 na zisizo za moja kwa moja 1800 hivyo kusaidia kukabiliana na changamoto ya ajira hasa kwa vijana nchini.
Naye Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango amesema kuwa PPF na Jeshi la Magereza lazima wahakikishe mipango waliyoiweka ya ujenzi wa kiwanda kipya na maboresho ya kiwanda cha zamani yanafanyika kwa wakati ili kwa haraka uzalishaji uanze na hatimaye nchi iweze kunufaika.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mhandisi Hamad Masauni ameishauri mifuko mingine ya pesheni kutumia fursa zilizopo Jeshi la Magereza ikiwamo maeneo na rasilimali watu katika kufikia azama ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati kupitia viwanda.
Akiongelea ujenzi wa kiwanda kipya Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni za wastaafu PPF, Bw.William Erio amesema kuwa kiwanda hicho kitagharimu shilingi bilioni 54.4 na kitakuwa na uwezo wa kuzalisha na wanategemea kuzalisha futi mraba za ngozi Milioni tatu laki saba na nusu (3,750,000/=) kwa mwaka.
Vilevile Bw. Erio amesema kuwa kiwanda hicho kitazalisha viatu vya kijeshi na kiraia jozi milioni moja na laki mbili kwa mwaka, pamoja na kutoa soli laki tisa kwa mwaka pamoja na kutoa bidhaa nyingine za ngozi kama mikanda,mabegi na mikoba ya akina mama takribani elfu arobaini na nane kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment