TANGAZO


Monday, July 17, 2017

Watu wawili wafa maji wakibatizwa Tanzania

Watu wawili wafa maji wakipatizwa Tanzania

Image captionWatu wawili wafa maji wakibatizwa Tanzania
Watu wawili wanaripotiwa kufariki wakati wakibatizwa siku ya Jumapili, kwenye mto ulio eneo la Rombo mkoa wa Kilimanjaro Kaskazini mwa Tanzania.
Kwa mujibu wa naibu kamanda wa polisi Hamisi Selemani Issa, watu hao walikuwa wakibatizwa kwa kuzamishwa ndani ya maji, katika zoezi lililokuwa likiendeshwa na mhubiri wa Kanisa la Shalom huko Rombo.
Walizama maji katika mto Ungwasi wakati walikuwa wakizamishwa baada ya kile kinachotajwa kwa kulemewa na mawimbi makali ya mto huo.
Haijulikani ni kwa njia gani mhubiri na waumini wengine waliokuwa wakiendesha zoezi hilo walinusurika.
Polisi baadaye waliitwa kuondoa maiti baada ya ajali hiyo.
Naibu kamanda wa polisi aliiambia BBC kuwa waumini wa kanisa akiwemo pia mhubiri wamezuiliwa ili kuhojiwa.

No comments:

Post a Comment