TANGAZO


Sunday, July 16, 2017

UJENZI BARABARA YA IPEMBE-MSONGOLE KUANZA MWEZI JUNI MWAKA HUU


Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akipata maeleozo ya mtandao wa ramani ya barabara za Mkoa wa Songwe kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Songwe Luteni Mstaafu Chiku Galawa wakati wa ziara yake ya kukagua barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM).
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (Kulia) akitoa maelekezo kwa kaimu Meneja wa Wakala wa barabara nchini (TANROADS)Mkoa wa Songwe Eng. Yona Kasaini (Kulia) alipokagua barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM) ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaanza mwezi juni  Mwaka huu.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani akipokea maoni ya  mkazi wa wilaya ya Ileje Mkoani Songwe wakati wa ziara yake ya kukagua  barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM) ambayo ujenzi wake kwa kiwango cha lami unaanza mwezi juni  Mwaka huu.  
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kulia) akitoa taarifa ya ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Ipemba hadi Msongole wilayani Ileje (50.3KM) kupitia radio Ileje Fm mara baada ya kukagua barabara hiyo, mkoani Songwe. 
Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya LEA International ltd, Canada akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (kushoto) kuhusu hatua iliyofikiwa ya ujenzi wa Barabara ya Mafinga-Nyigo KM 74.1 wakati Eng. Ngoyani alipokagua maendeleo ya mradi huo Mkoani Njombe. 
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Eng. Edwin Ngonyani (wa pili kushoto) akitoa maelekezo kwa Mhandisi Mshauri kutoka Kampuni ya LEA International ltd, Canada kuhusu kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara Mafinga-Nyigo KM 74.1 wakati alipokagua maendeleo ya mradi huo Mkoani Njombe.

SERIKALI imetenga kiasi cha sh. bilioni 107.56 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara ya Ipemba hadi Isongole wilayani Ileje yenye urefu wa kilomita 50.3 kwa kiwango cha lami ili kuunganisha Mkoa wa Songwe na nchi jirani ya Malawi.

Naibu Waziri  wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, Eng. Edwin Ngonyani ametoa kauli hiyo mara baada ya kukagua barabara hiyo ambapo amesema ujenzi huo utaanza mwezi juni  Mwaka huu na kukamilka mwezi June, 2019.

"Tayari mkandarasi  ameshapatikana na sasa ameanza kufanya maandalizi ya kuleta vifaa vitakavyotumika katika ujenzi huu, Serikali ya Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kukamilisha ahadi hii kwa miezi ishirini na nne toka pale ujenzi utakapoanza". amesema Eng. Ngonyani.

Aidha, Eng. Ngonyani amesema  kuanza kwa ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami ni katika hatua za  kutekeleza ahadi iliyotolewa na Serikali kwa wanachi wa mkoa huu katika vipindi tofauti tofauti vya uongozi.

"Wananchi wa hapa wana shauku kubwa na barabara hivyo kukamilika kwake kutasaidia kuufungua mkoa huu kwa upande wa Malawi ambao tunapakana nao na hivyo kukuza shughuli za kibiaahara baini ya nchi hizi mbili na kupelekea kukuza uchumi kwa wakazi hawa," amesisitiza Eng Ngonyani.

Naye Meneja wa Wakala wa barabara nchini (TANROADS) mkoa wa Songwe amemuhakikishia Waziri Ngonyani kuwa wakala utasimamia ujenzi huo ili ukamilike kwa wakati na viwango vinavyokubalika," amesema Eng. Yona Kasaini.

"Barabara hii itajengwa kwa kiwango  cha lami ya daraja la  kwanza ili kuiwezesha kudumu kwa muda mrefu zaidi, sisi tutahakikisha kazi hii inakamilika kwa mujibu wa makubaliano yaliyopo kwenye mkataba wetu,” amesema Eng.Yona Kasaini.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Songwe Bi. Chiku Galawa ameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuamua kujenga barabara hii na ameahidi kutoa ushirikiano kwa TANROADS na mkandarasi wa M/s China Engineering Corporation atakayejenga barabara hiyo.

Katika hatua nyingine Eng. Ngonyani amekagua mradi wa  ukarabati wa barabara ya Mafinga-Nyigo (74.1 KM) na kipande cha Nyigo-Igawa (63.8 KM) ambapo amemtaka mkandarasi anayejenga barabara hiyo kuongeza kasi ya ujenzi wa barabara hiyo.
“Ninakuagiza baada ya miezi miwili nitarudi hapa nikute ujenzi umefikia asilimia 65 sababu mmeshindwa na kasi tunayoitaka wakati fedha mmepewa,” alisisitiza Eng. Ngonyani.

Kwa upande wake Meneja Mradi kutoka Kampuni ya China Civil Engineering CONsturtcion Corporation (CCECC), Bw. Martin Bai amemuhakikishia Eng. Nyongani kuwa watakwenda na kasi kwani wameongeza idadi ya vifaa vya kufanyia kazi na kuahidi atakaporudi ataona maendeleo makubwa.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments:

Post a Comment