Mwanasiasa mmoja nchini Brazil amewakashifu waandamanaji wa mrengo wa kushoto kwa kuwadhulumu wageni wakati wa harusi yake kufuati familia yake kumuunga mkono Rias Michel Temer.
Maria Victoria Barros, 25, ni mbunge huko Panara na bintiye waziri wa afya nchini Brazil
Mamia ya waandamanaji walikusanyika nje ya kanisa ambapo sherehe zilikuwa zikifanyika siku ya Ijumaa jioni.
Waandamanaji hao walirusha mayai na mwanasiasa hiyo akalamizimika kuondoka akitumia gari lisilopenya risasi
- Rais wa zamani wa Brazil ahukumiwa miaka tisa jela
- Michel Temer: sitojiuzulu kwa kashfa ya rushwa
- Majaji Brazil kupiga kura ya kumuondoa Rais Temer
- Jaji wa mahakama kuu afariki kwenye ajali Brazil
Sherehe hiyo ilihuduriwa na wanasiasa wa nchi hiyo, akiwemo babake Ricardo Barros na mamake Cida Barghetti naibu gavana wa Parana.
Takriban wabunge 30 wa nchi hiyo waliakikwa kusafiri kutoka mji mkuu Brasilia kuhudhuria harusi kwenye mji mkuu wa jimbo la Parana Curitiba.
Picha katika mtandao wa You Tube zinaonyesha walinzi walifungua miavuli kuwakinga binti na bwana harusi walipokuwa wakiondoka kanisani.
No comments:
Post a Comment