TANGAZO


Friday, July 14, 2017

Man City wakamilisha kumnunua Kyle Walker kutoka Tottenham

Kyle Walker

Haki miliki ya pichaAFP
Image captionKyle Walker amechezea England mechi 27
Manchester City wamekamilisha ununuzi wa beki wa kulia wa Tottenham na England Kyle Walker kwa kitita cha £45m.
Walker, ambaye amechezea taifa lake mechi 27 na amekuwa na Spurs kwa msiimu minane, ametia saini mkataba wa miaka mitano City.
Uhamisho wake, ambao unakuwa na jumla ya £50m ukiongeza kikolezo cha £5m, huenda ukamfanya kuwa mchezaji ghali zaidi wa England kuwahi kuwepo.
"Nina furaha sana kujiunga na City na nasubiri sana kuanza kucheza," amesema Walker.
"Pep Guardiola ni miongoni mwa mameneja wanaoheshimiwa zaidi duniani."
Walker alijiunga na Spurs kutoka Sheffield United mwaka 2009 na amecheza mechi 183 Ligi ya Premia.
Katika Manchester City atavalia jezi nambari mbili.
Anatarajiwa kusafiri na City Jumatatu kwa ziara yao ya Marekani.

Wachezaji ghali zaidi wa Uingereza

£85.3m - Gareth Bale (Tottenham kwenda Real Madrid, 2013)
£49m - Raheem Sterling (Liverpool kwenda Manchester City, 2015)
£47.5m - John Stones (Everton kwenda Manchester City 2016)
£45m - Kyle Walker (Tottenham kwenda Manchester City 2017)
£35m - Andy Carroll (Newcastle kwenda Liverpool, 2011)

No comments:

Post a Comment