TANGAZO


Monday, May 1, 2017

Sulley Muntari apewa kadi ya manjano akilalamikia kubaguliwa

Sulley Muntari akiwajiu mashabiki wakati wa mechi

Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSulley Muntari akiwajiu mashabiki wakati wa mechi
Mchezaji wa Pescara Sulley Muntari, aliondoa uwanjani baada ya refa kumpa kadi ya manjano, alipolalamika kuwa alikuwa akidhulumiwa kwa misingi ya rangi wakati wa mechi.
Kiungo huyo wa zamani wa Ghana mwenye umri wa miaka 32, alimuomba refa Daniele Minelli asimamishe mechi hiyo ya Jumapili.
Lakini badala yake refa alimpa kadi ya manjano dakika ya 89, hatua iliyosababisha mchezaji huyo wa zamani ya vilabu vya Portsmouth na Sunderland kupinga kwa kuondoka uwanjani.
Kwa hasira aliwakabili mashabiki wa klabu ya Cagliari akisema kwa sauti. "Hii ni rangu yangu."
Sulley Muntari akiongea na refa wakati Pescara ilishindwa na CagliariHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSulley Muntari akiongea na refa wakati Pescara ilishindwa na Cagliari
Akiongea baada ya mechi Muntari alisema: "Refa hastahili kukaa tu uwanjani na kupiga firimbi, ni lazima afanye kila kitu.
"Ni lazima aone vitu hivi na kuonyesha mfano.
"Nilimuuliza ikiwa alikuwa amesikia matusi. Nikasisitiza kuwa ni lazima asimamishe mechi."
Meneja wa Pescarfa Zdenek Zeman ambaye upande wake ulishindwa kwa bao 1-0, alisema kuwa alimuomba refa kuingilia kati lakini akasema hakuona wala kusikia chochote.

No comments:

Post a Comment