Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017. (Picha na IKULU)
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimsindikiza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein walipokutana kwa mazungumzo Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma leo Jumatatu Machi 13, 2017.
Ikulu, Dodoma.
RAIS wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 13 Machi 2017,
amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein Ikulu ya Chamwino mjini Dodoma.
Dkt. Magufuli
amesema katika mazungumzo yao wamezungumza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na
kumtakia heri Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali
Mohamed Shein kufuatia leo kuwa siku yake ya kuzaliwa.
Kwa upande wake
Rais Dkt. Ali Mohamed Shein amesema anamshukuru Rais Dkt.Magufuli kwa kumtakia
heri katika siku yake muhimu ya kuzaliwa na hivyo wamekutana kubadilishana
mawazo katika kuhakikisha wanajenga nchi na kusonga mbele.
''Siku ya kuzaliwa
ni siku ya furaha lazima ikumbukwe lazima isherehekewe, mimi siku yangu ya
kuzaliwa sisherehekei sana lakini huwa nafurahi sana na leo nimefurahi sana''
amesema Dkt. Shein.
Dkt.Shein amesema
ametumia siku yake ya kuzaliwa kumtembelea Rais Dkt.Magufuli ili waweze
kubadulishana mawazo kwani wana kazi kubwa ya kujenga nchi.
Jaffar
Haniu
Naibu Mkurugenzi
wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dodoma
13 Machi,
2017
No comments:
Post a Comment