Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu kazi Vijana na Ajira Mhe. Anthony Mavunde akiwapongeza vijana wa Jogging club na wakazi wa Dodoma kwa kushirki michezo mara baada ya kufanya mazoezi ya pamoja yenye nia ya kuimarisha afya na kuendeleza michezo nchini yaliyofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma leo March 1, 2017.
Picha zote na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM, Dodoma
02/03/2017
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye pamoja na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Mhe. Anthony Mavunde wameamua kuchukua jukumu la kuwa walezi wa vikundi vya Jogging vilivyopo Dodoma.
Azma hiyo imetolewa jana Mjini Dodoma na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye alipokuwa akizungumza na vijana kutoka vikundi vya Jogging mbalimbali Dodoma alipokutana nao na kushiriki mazoezi katika Uwanja wa Jamhuri.
Mhe. Nape Nnauye alisema kuwa watahakikisha kuwa kila mtaa unakuwa na kikundi cha Jogging ili kuleta hamasa ya michezo na Utamaduni wa kufanya mazoezi.
“Mimi na Mhe. Naibu Waziri Mavunde tutakuwa walezi wenu kwani ukikaa karibu na ua waridi lazima utanukia” alisistiza Mhe. Nnauye.
Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Ajira na Vijana Mhe. Anthony Mavunde ametoa wito kwa vijana wa Dodoma kujitokeza kwa wingi kujiungana vikundi vya Jogging ili kuendeleza na kukuza Utamaduni wa michezo nchini.
“Niwaombe vijana wa Dodoma wajiunge na vikundi vya Jogging na kujihusisha na masuala ya michezo ili wakuze vipaji vyao na kujenge Utamaduni wa michezo” Alisisitiza Mhe. Mavunde.
Aidha mmoja ya mwanachama wa kikundi cha Jogging ya Muungano Bw. Zebedayo Marko amesema kuwa wamefarijika sana na viongozi wao kujitoa kuwa walezi wa Klabu za Jogging Dodoma kwani itasaidia kuleta hamasa kwa vijana wengi kujihusisha na michezo.
Baada ya tamko kutoka kwa viongozi hao sasa vikundi vya Jogging Dodoma zitafadhiliwa vifaa vya michezo na mahitaji yote yahusuyo mazoezi kwa klabu hizo.
No comments:
Post a Comment