TANGAZO


Monday, March 6, 2017

Mzozo wa dhahabu wasababisha watu 4 wa familia moja kuuawa Ufaransa

Familia ya Troadec ilionekana mara ya mwisho tarehe 16 mwezi Februari mwaka huuHaki miliki ya pichaAFP
Image captionFamilia ya Troadec ilionekana mara ya mwisho tarehe 16 mwezi Februari mwaka huu
Ndugu wa watu wanne wa familia moja ambao wamekuwa hawajulikani waliko nchini Ufaransa tangu kati kati ya mwezi Februari amekiri kuwa ndiye aliwaua.
Aliyekuwa shemeji wa familia ya Pascal Troadec kwa jina Hubert C, anaripotiwa kuwaambia wachunguzi kuwa aliwaua kutokana na mzozo wa umiliki wa dhahabu.
Inaamiwa kuwa aliwaua kwa kuwapiga kwa kifaa butu nyumbani kwao eneo la Nantes, kwa mujibu wa gazeti la Le Parisien.
Chembechembe zake za DNA zinaripotiwa kupatikana kwenye nyumba ya watu hao.
Dadake Pascal Troadec na shemeji wake wa zamani wanahojiwa BrestHaki miliki ya pichaAFP/GETTY
Image captionDadake Pascal Troadec na shemeji wake wa zamani wanahojiwa Brest
Alikamatwa pamoja na dadake Troadec, ambaye ni mke wake wa zamani eneo la Brest, na vyombo vya habari vinasema kuwa bidhaa za familia hiyo vilipatikana eneo hilo.
Pascla na Brigitte wote wenye umri wa miaka 49, mtoto wao wa kiume Sebastien 21, na binti yao Charlotte 18, walionekana mara ya mwisho Februari tarehe 16.
Haijaripotiwa ikiwa Hubert C, amewaambia polisi ilipo miili yao.
Mzozo huo wa urithi unaripotiwa kuzuka kutokana na dhahabu iliyopatikana wakati wa ukarabati wa nyumba eneo la Brest, iliyomilikiwa na baba yake Troadec ambaye alifariki miaka kadha iliyopita.
Ramani ya Nantes, Brest na Saint-Nazire nchini Ufaransa
Image captionRamani ya Nantes, Brest na Saint-Nazire nchini Ufaransa
Bidhaa za Charlotte zilipatikana eneo lenye mitiHaki miliki ya pichaAFP
Image captionBidhaa za Charlotte zilipatikana eneo lenye miti

No comments:

Post a Comment