Rais wa Tanzania John Magufuli ameagiza kampuni ya simiti ya Dangote kupewa ruhusa ya kuchimba mkaa wa mawe nchini humo ili iweze kuutumia kwenye kiwanda chake kilicho mtwara kwa mujibu wa gazeti la The Citizen.
Dr Magufui aliliamrisha shirika la maendeleo ya taifa NDC kuipa kampuni hiyo sehemu ya mgodi wa mkaa wa mawe wa Ngaka ulio wilaya ya Mbinga.
Rais Magufuli alitoa agizo hilo kabla ya kuzindua malori 580 ambayo yatatumiwa kusafirisha simiti kutoka kwenye kiwanda hadi sehemu tofauti za nchi.
Magufuli anasema anafahamua kuwa uzalishaji wa simiti kwenye kiwanda hicho umekuw aukikumbwa changamoto kadha.
Aliongeza kuwa uchimbaji uliokuwa ukifanywa na kampuni iliyokuwa imepewa kandarasi ya Tancoal Energy Limited ulikuwa duni.
"Chini ya makubaliano ni vigumu kuhakikisha kuwa muwekezaji anapata mkaa wa mawe wa kutosha kwa uzalishaji wa simiti kwa sababu ya uzalishji mdogo wa mkaa.
"Kwa hivyo mumpe Dangote kipande cha ardhi kwenye mgodi ili apate kuchimba mkaa kwa kiwanda chake," alisema Rais Magufuli, akiimaanisha tajiri raia wa Nigeria Aliko Dangote, ambaye pia alihudhuria sherehe hizo.
Bwana Dangote ni mwanzilishi na mkurugenzi mkuu ya kampuni ya Dangote Group, ambayo inamiliki kiwanda cha simiti cha Mtwara.
No comments:
Post a Comment