TANGAZO


Tuesday, March 14, 2017

MMILIKI WA UJIJIRAHAA BLOG ASHEREHEKEA SIKU YA KUZALIWA NA MADAKTARI WA KINYWA NA MENO KATIKA HOSPITALI YA MKOA SHINYANGA


Mmiliki wa Ujiji Rahaa Blog, Khamisi Bilali (wa pili kushoto) akishirikiana kukata Keki ya kuashiria siku ya kuzaliwa kwake na Madaktari wa Chama Cha Mdaktari wa Kinywa na Meno Mkoani Shinyanga katika Hospitali ya Mkoa huo wakati walipofika kupata chakula cha mchana jana, wa tatu kushoto ni  Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salamu, Conrad Mselle  na wakwanza kushoto ni Daktari wa Meno Wilaya ya Ngara Mkoa wa Kagera, David Mapunda.
Mmiliki wa Blog ya Ujijirahaa, Khamisi Bilali akimlisha keki Daktari Bingwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Habiba Madjapa (kushoto) hafla hiyo iliyofanyika katika Hospitali ya Mkoa Shinyanga leo mara baada ya kupata chakula cha mchana.   
Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salamu, Conrad Mselle (kulia) wakilishana Keki na Mmiliki wa Ujijirahaa Blog katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake Khamisi Bilali Mkoani Shinyanga jana, kushoto anaye shuhudia ni Daktari Bingwa Hospitali ya Taifa Muhimbili,  Dr. Arnold Mtenga



Mmiliki wa Ujijirahaa Blog katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake Khamisi Bilali (kulia) akimlisha Keki,  Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya hafla iliyofanyika  Mkoani Shinyanga jana.
Mmiliki wa Ujijirahaa Blog katika kuadhimisha siku ya kuzaliwa kwake Khamisi Bilali (kulia) akimlisha Keki, Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno, Tanzania Dr Lorna CarneiroMkoani Shinyanga jana.

Siku ya kuzaliwa tarehe kama yaleo, Machi 13 ndiyo siku ambayo Mungu alipanga niingie Ulimwenguni hivyo ninazidi kumuomba Mungu maisha mema na yenye faraja azidi nijalia na yenye mwisho mwema, alisema Bilali,

Dua nyingi ziwafikie wazazi walionileta Duniani na malezi wakanipa na kufikia hapa lipofikia na si kwa ujanja wangu zaidi ni Mungu anipe mwisho mwema na nizidi kuwakumbuka walionileta Duniani Dua ziwafikie popote walipo japo Baba yangu ametangulia mbele ya haki 

Dua namuombea alisema Bilali,  hekima, busara na weledi ninguzo mojawapo ya maisha na Unapoamka salama basi mshukuru Mungu kwani kuna mamilion ya watu wamepoteza maisha, wamepata matatizo mbali mbali na kujikuta wanaamkia wengine hospitali.

Ukishaamka ili uwe makini na utakachofanya leo, jikumbushe yoote uliyofanya jana, kama kuna mazuri weka ahadi ya kuyaendeleza, na kama yapo uloteleza basi chukia na kuweka ahadi ya kutoyafanya tena Kwani huwezi kusonga mbele kama hukumbuki ulikotoka, niwatakie mwanzo mwema wa wiki.

No comments:

Post a Comment