Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela akizungumza na madaktari wa Kinywa na Meno kutoka sehemu mbalimbali wakiwemo kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam (pichani hawapo) wakati walipofika Ofisini kwake na kujitambulisha katika kuelekea Maadhimisho ya siku ya Wiki ya Kinywa na Mane ambapo kilele ni machi 20, Dodoma na anatarajiwa mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana, ambapo Katibu Tawala huyo alisema, napenda kutowa shukrani za kipekee na kwaniaba ya Mkoa wangu kwa jinsi mnavyo jitowa katika kuwahudumia ndugu zetu, watoto wetu na mgeweza kwenda sehemu nyingine lakini kwa mfululizo wa miaka mitatu mnakuja kututembelea na kutowa huduma, misaada na elimu ya jinsi ya kutunza afya ya kinywa na meno na sasa kunamabadiliko makubwa tofauti na mara yakwanza mlipofika na baada ya hapo wengi walijitokeka katika kusaidia watoto hao, nawaombea kwa Mungu mpate kuja kututembelea kwa mara nyingine, karibuni sana hapa ni kwenu na msisite kuniona na pia nitafika kuja kuwaona kabla hamjafunga huduma hiyo. hayo aliyasema leo ofisini kwake baada ya kutembelewa na Madaktari wa afya ya meno walipomtembelea ofisini kwake katika kuelekea Maadhimisho ya wiki ya kinywa na meno.(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Madaktari wa Kinywa na Meno wakikaribishwa na watoto wa Shule ya Msingi Buhangija Mkoani Shinyanga kwa wimbo.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jumuishi ya Kata ya Buhangija Mkoani Shinyanga wakifurahia jambo.
|
Daktari Bingwa wa Kinywa na Meno Hospitali ya Taifa Muhimbili Dar es Salamu, Conrad Mselle akitowa Elimu ya upigaji mswaki wa Kinywa na Meno leo mbele ya wanafunzi wa shule hiyo katika kuelekea kilele cha Maadhimisho yatakayofanyika machi 20, mwaka huu Dodoma, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mkuu wa Mkoa, Jordan Rugimbana.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dr. Lorna Carneiro akizungumza na wanafunzi hao.
Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya akifungua wiki ya kinywa na Meno leo katika Shule ya Wanafunzi wa Shule ya Msingi Jumuishi ya Kata ya Buhangija Mkoani Shinyanga.
Maktari Bingwa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Habiba Madjapa (kulia) na Dr Arnold Mtenga (katikati) wakijadiliana na Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno, Tanzania Dr. Lorna Carneiro (kushoto).
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (wa nne kulia) akiwa katika picha ya pamoja na madaktari hao.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (kulia ) akikabidhiwa flana na Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno Tanzania, Dr. Lorna Carneiro mara walipofika na msafara wake kwa lengo la kujitambulisha.
Rais wa Chama cha Madaktari wa Kinywa na Meno, Tanzania Dr Lorna Carneiro (kushoto) akizngumza jambo wakati walipofika yeye na msafara wake kumsalimia Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (kulia) katikati ni Daktari wa Meno Mkoa wa Shinyanga, Dkt. Nuru Mpuya.
Katibu Tawala Mkoa wa Shinyanga, Albert Msovela (katikati aliyevaa koti) akizungumza na madaktari hao (kulia ).
No comments:
Post a Comment