Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia
Profesa Joyce Ndalichako akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya
ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) jana Jijini Dar es
Salaam. Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki na Kaimu
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Dkt. Bwire
Ndazi. (Picha zote na Frank Shija – Maelezo)
Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) Peter Maduki akizungumza mara baada ya Bodi ya uzinduzi wa rasmi wa Bodi hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi. Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi akizungumza mara baada ya Bodi ya uzinduzi rasmi wa Bodi hiyo jana Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako na Mwenyekiti wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) Peter Maduki (kushoto).
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya
Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa
Bodi hiyo jana Jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi wakifuatilia hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akimkabidhi taarifa ya utekelezaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) Mwenyekiti Mpya wa Bodi ya Mamlaka hiyo, Peter Maduki wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akimpa maelekezo Mwenyekiti Mpya wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board), Peter Maduki (kulia) mara baada ya kumkabidhi taarifa ya utekelezaji wa Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo jana Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia,
Profesa Joyce Ndalichako akimsikiliza mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Mamlaka ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) kupitia Bakwata Suleiman Lolila
(kulia) mara baada ya kuzindua Bodi hiyo jana, Jijini Dar es Salaam. Katikati ni
Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo Peter Maduki (katikati).
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wajumbe wa Bodi Mpya ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET – Board) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Bodi hiyo jana, Jijini Dar es Salaam. Waliokaa kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa VETA Dkt. Bwire Ndazi na Kushoto ni Mwenyekiti Mpya wa Bodi, Peter Maduki.
Na Frank Shija,
Maelezo.
BODI ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) imeagizwa kuanza mara moja kutekeleza
miradi ya maendeleo ambayo utekelezaji wake umekuwa ukisuasua kwa muda mrefu
huku kukiwa na fedha zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji miradi hiyo.
Agizo hilo limetolewa
na Waziri wa Elimu, Sayansi na wakati akizindua Bodi Mpya ya Elimu, Sayansi na
Teknolojia ya Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VET –Board) jana Jijini Dar es Salaam.
Profesa Ndalichako
ameshangazwa na kitendo hicho cha ucheleweshaji wa utekelezaji wa miradi hiyo
huku kukiwa na shilingi takribani bilioni 14.5 zilizotengwa katika bajeti ya
mwaka wa fedha 2016/207 kwa ajili ya kazi hizo.
“Inasikitisha kuona
kuwa tunakaribia robo ya mwisho ywa mwaka wa fedha 2016/2017, huku karibu
miradi yote ya maendeleo haijaanza kutekelezwa,isipokuwa ile tu ya kujengea
uwezo na siyo ya ujenzi wa VETA ambazo ndiyo hitaji kubwa kwa sasa.”Alisema
Profesa Ndalichako.
Ndalichako ameongeza
kuwa Bodi hiyo inapaswa kuanza kazi mara moja ikiwa ni pamoja na kuwachukulia
hatua watendaji watakao bainiuka kuhusika katika ucheleweshaji wa kuanza kwa
miradi hiyo.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa Bodi hiyo Peter Maduki amempongeza Waziri Ndalichako kwa kuwa
muwazi katika kuelezea kutolridhishwa na udhaifu katika utendaji kwa baadhi ya
wafanyakazi wa Mamlaka hiyo na kuahidi kushughulikia suala hili huku akiwataka wajisahihishe
badala ya kusubiri kuwajibishwa.
“Mhe Waziri, maelekezo
yako tumeyapokea, nikuahidi tu kuwa mimi pamoja na timu yangu tutayafanyika
kazi, ni nisememe wazi tupo tayari kushirikiana nawe wakati wowote,” alisema
Mduki.
Awali akisoma maelezo
mafupi kuhusu Bodi ya Mamlaka hiyo wakati, Kaimu Mkuu wa Mamlaka ya Elimu na
Mafunzo ya Ufundi Stadi(VETA) Dkt. Bwire Ndazi amebainisha changamoto kadhaa
katika eneo hili la utoaji wa elimu na mafunzo ya ufundi stadi kuwa ni pamoja
na uwezo mdogo wa VETA na wadau katika kufikia mahitaji ya elimu na mafunzo ya
ufundi akitolea mfano kuwa watu wanaohitaji kujiunga na mafunzo wanakadiriwa
kuwa laki sita kwa mwaka, uwezo wa vyuo vyote vya VETA, VYA Serikali na binafsi
ni kati ya 125,000 tu kwa mwaka.
Bodi iliyomaliza muda
wake iliundwa Agosti 2011 na kumaliza muda wake kisheria Agosti 2014, na
baadaye kuongezewa muda hadi desemba
2016 alipoteuliwa Mwenyekiti Mpya wa Bodi hiyo yenye jumla ya wajumbe 10
kutoka maeneo ya ujuzi mbalimbali.
No comments:
Post a Comment