Kauli ya Waziri Nape ameitoa leo asubuhi wakati akifungua mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari kuelekea Anfield ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi katika viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani. Alisema haiwezekani taifa hili kuwa na Waziri mjanja kama Nape halafu Serengeti Boys inakosa kombe huko Gabon na nafasi ya ushiriki Kombe la dunia. Pamoja na kauli yake hiyo Waziri Nape aliiomba Benki ya Standard Chartered kushiriki katika jukumu la kuhakikisha kwamba Serengeti Boys ama inarejea na kombe au inafuzu miongoni mwa timu mbili zitakashiriki Kombe la Dunia.
Picha juu na chini ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati), Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (mwenye kofia) na Mwenyekiti wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama (wa tatu kulia) wakijumuika kwa pamoja na washiriki wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) kutoka makampuni mbalimbali kupasha misuli moto yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.(Picha na thebeautytz.co.tz)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati), Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (mwenye kofia) na Mwenyekiti wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama (kushoto kwa Waziri Nape) katika picha ya pamoja baada ya kukabidhi bendera kwa washiriki kutoka makampuni mbalimbali wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani akisoma risala kwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (hayupo pichani) wakati wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Aliitaka Benki hiyo kuendelea kufadhili michezo nchini ili iweze kukua.
Wakati huo huo Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani Sanjay amesema kwamba benki yake inaona fahari kuwa mgeni wa michuano hiyo kuelekea Anfield kwa nchi za Afrika Mashariki na kuwataka washiriki wakaze nia ya kutwaa ubingwa.
Alisema mashindano ya mwaka huu yanaendana na miaka 100 ya shughuli za benki hiyo nchini Tanzania.
Mwenyekiti wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye kubariki mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Mgeni rasmi Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizungumza na washiriki wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) akibadilishana mawazo na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani wakati mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) yakiendelea katika viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye akizundua rasmi mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari kuelekea Anfield kwa kupiga mpira kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Mchezaji wa Benki ya Standard Chartered (jezi nyeupe) akichuana vikali na wenyeji wa JK Park (jezi za kijani) kwenye mechi ya kwanza ya dakika kumi wakati wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 ya safari kuelekea Anfield ambapo timu ya JK Park iliibuka kidedea kwa bao 1-0.
Mchezaji wa Mwananchi Communication (tisheti nyeupe) akijaribu kumtoka mchezaji wa ORYX kwenye wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 safari kuelekea Anfield ambapo timu ya ORYX Park iliibuka kidedea kwa bao 2-0.
Mshehereshaji wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield), Maulid Baraka wa Kitenge (kulia) akibadilishana mawazo na Meneja Miradi wa Executive Solutions, Hilda Ngowi (katikati) na Mhasibu wa Executive Solutions, Mapunda (kushoto) wakati wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkuu wa kitengo cha makampuni makubwa wa benki hiyo, Jaffer Machano wakati wa mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye (katikati) kwenye picha ya pamoja na Mtendaji Mkuu wa Benki ya Standard Chartered, Tanzania Sanjay Rughani (wa pili kushoto), Mkuu wa kitengo cha makampuni makubwa wa benki hiyo, Jaffer Machano (wa pili kulia), Mwenyekiti wa Kamati ya uamuzi TFF, Salum Chama (kulia) na Mkuu wa Mahusiano na Masoko wa Benki ya Standard Chartered, Juanita Mramba (kushoto) wakati mashindano ya Kombe la Standard Chartered 2017 (Road to Anfield) ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 100 tangu benki hiyo kuanzishwa mwaka 1917 yaliyoanza kutimua vumbi leo kwenye viwanja vya JK Park Kidongo Chekundu, Gerezani jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment