Muonekano
wa Kiwanja cha ndege cha Masasi, ambacho kina uwezo wa kuhudumia ndege za
abiria saba mpaka kumi.
SERIKALI imesema itatuma wataalam wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini (TAA),
kuangalia Maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya Ujenzi wa Viwanja vya ndege katika Wilaya
ya Masasi na Tunduru ili kujiridhisha na kushauri Serikali namna ya kutekeleza miradi
hiyo.
Akizungumza
mara baada ya kuonyeshwa maeneo hayo Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano
Prof. Makame Mbarawa amesema pamoja na maeneo hayo kutengwa na Wilaya hizo kuna
ulazima wa kuwatuma wataalam wa Viwanja ili kuwa na Viwanja bora
vinavyozingatia viwango vya kimataifa.
“Nawapongeza
sana kwa kutenga maeneo kwa ajili ya kujengaViwanja vya ndege kwani ni muhimu sana
kwa maendeleo ya nchi, hivyo ili kukidhi viwango vilivyowekwa kimataifa katika
ujenzi wa viwanja vya ndege nitatuma wataalam
kutoka TAA ili kukagua maeneo haya na watoe muelekeo kwa kuishauri Serikali kuhusu
utekelezaji wa miradi hii muhimu”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Kuhusu
kiwanja cha Masasi Waziri Mbarawa ameiagiza TAA na Halmashauri ya Wilaya yaMasasi
kukaa pamoja na kuainisha mipaka ya kiwanja hicho ili kuepuka uvamizi wa
miundombinu ya kiwanja hicho.
Aidha,
Waziri Prof. Mbarawa amemuagiza Mkuu wa Wilaya hiyo kuiandikia Wizara mahitaji
ya eneo hilo na kuainisha sababu ya kuhamisha kiwanja cha ndege cha Tunduru kutoka
mjini kwenda nje ya mji.
Kwa
upande wake, Kaimu Meneja
wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), mkoani Mtwara, Bi. Zitta
Majinge, amemhakikishia Waziri huyo kuleta maombi ya mapendekezo ya viwanja
hivyo makao makuu ili kuweza kutafutiwa ufumbuzi wa changamoto za viwanja
hivyo.
(Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano)
No comments:
Post a Comment