Mwanasheria mkuu wa Malaysia, anasema wanawake wawili wanaodaiwa kumuua ndugu wa kambo wa rais wa Korea kaskazini Kim Jong Un watashtakiwa kwa makosa ya mauaji.
Wawili hao, raia wa Indonesia na Vietnam wanakabiliwa na hukumu ya kifo, kwa mauji ya Kim Jong Nam katika uwanja wa ndege mjini Kuala Lumpar.
Malaysia inasema, Bwana Kim aliyekuwa mkosoaji wa nduguye, aliuwawa kwa kutumia sumu aina ya VX, ambayo imepigwa marufuku na Umoja wa mataifa.
Washukiwa hao wawili wanadaiwa kumpaka usoni kemikali hiyo ya sumu katika uwanja wa ndege wa Malaysia mapema mwezi huu.
Wamesema kuwa walidhani walikuwa wakifanya mzaha katika filamu.
- Mwili wa Kim Jong-nam walindwa vikali
- Kifo cha Kim: Mwanamke akamatwa Malaysia
- Korea Kaskazini ndiyo ilimuua Kim Jong-nam, yadai Korea Kusini
Watashtakiwa chini ya sheria ambapo iwapo watapatikana na hatia watanyongwa.
Hatahivyo hakuna hatua iliochukuliwa kuhusiana na kumshataki raia wa Korea Kaskazini ambaye pia anazuiliwa kwa muaji hayo.
- Wanawake hao ni Doan Thi Huong, mwenye umri wa 28, kutoka Vietnam na Siti Aisyah, mwenye umri wa 25, kutoka Indonesia na ni miongoni mwa washukiwa 10 waliotambuliwa na Malaysia kwamba huenda walihusika na mauaji hayo.
- Mshukiwa wa mauaji ya Kim Jong nam akamatwa
- Watu zaidi wakamatwa kufuatia kifo cha Kim Jong-nam
Washukiwa hao ni pamoja na afisa mkuu katika ubalozi wa Korea Kaskazini mjini Kuala Lumpur pamoja na mfanyikazi mmoja wa kampuni ya ndege ya taifa hilo.
Korea Kusini inaamini kwamba washukiwa wanne ni wapelelezi wa Korea Kaskazini.
No comments:
Post a Comment