Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Adam Mayingu, (kushoto), akizungumza jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa benki ya CRDB, Dkt. Charels Kimei, wakati wa uzinduzi wa ushirikiano baina ya taasisi hizo mbili ambapo CRDB sasa itawakopesha Wanachama wa PSPF kwenye maeneo ya elimu, viwanja na pesa za kuanzia maisha kwa watumishi wa serikali. Uzinduzi huo umefanyika Februari 27, 2017 makao makuu ya PSPF jijini Dar es Salaam.
NA
K-VIS BLOG
WANACHAMA
wa mfuko wa pensheni wa PSPF sasa Wwataanza kupata mikopo yao kupitia benki ya
CRDB mara baada ya kuzinduliwa kwa
mpango huo baina ya taasisi hizo mbili jana jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza
kwenye hafla ya utiaji saini mpango huo
, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Bw
Adam Mayingu , alisema kuwa mpango huo wa kutoa mikopo kwa wanachama ulianza
tangu Desemba 2014 kwa kupitia taasisi nyingine za kifedha.
Alisema
kuwa PSPF na benki ya CRDB wamekubaliana
kushirikiana katika kuendesha kwa pamoja huduma ya mikopo.
Mikopo
hiyo ni pamoja na mkopo wa elimu(education loan scheme), mkopo wa kuanzia
maisha( startup life loan scheme) na mkopo wa viwanja(Nipo site na PSPF).
Alisema
kuwa kwa upande wa mkopo wa elimu mwanachama anaweza kukopa kwa ajili ya
kujiendeleza kielimu katika ngazi yeyote ya elimu .Ngazi hiyo ni stashahada, shahada, shahada ya uzamili na
hata mafunzo ya ufundi.
Kwa
upande wa mkopo wa kuanzia maisha, alisema kuwa mwanachama aliyepata ajira kwa mara
ya kwanza huwa na mahitaji yake muhimu
na kwa kutambua hilo, PSPF kwa kushirikiana na CRDB wameanzisha mpango huu ambapo mwanachama anaruhusiwa
kukopa mishahara yake ya miezi miwili ili awaeze kujipanga na maisha mapya ya
ajira.
Kuhusu
mkopo wa viwanja kwa wanachama, alisema kuwa
huduma hii itawawezesha wanachama wa PSPF kukopa na kumiliki viwanja vya
makazi ambavyo vinapataikana maeneo
mbali mbali ya nchi.
“Lengo kubwa hapa ni kuwawezesha wanachama wa PSPF
kumiliki viwanja vya makazi vilivyopimwa iii kuwaepusha dhdi ya ujenzi katika
makazi holela, ambayo yamekuwa na gharama kubwa kuliko makazi
yaliyopangiliwa”,alisema.
Alifafanua
kuwa lengo kubwa la kuanzisha mikopo hiyo ni kuhakikisha kila mtanzania
anatimiza ndoto yake ikiwa ni katika
masomo kupitia mkopo wa elimu , ndoto
yake nyingine kupitia mkopo wa kuanzia maisha au mkopo wa viwanja.
Hadi
kufikia tarehe 17 Mwezi huu idadi ya wanachama walionufaika na mikopo hiyo na idadi kwenye mabano ni Elimu (1,432)),
mkopo wa kuanzia maisha ( 847), mkopo wa viwanja (58).
“Kwa
kushirikiana na benki ya CRDB ambayo ina mtandao mkubwa wa matawi hapa nchini
tunaamini watanzania wengi watanufaika na mikopo hii na kwa kufanya hivyo
tutakuwa tunatakeleza juhudi za serikali ya awamu ya tano ya kuhakikisha
watanzania wengi zaidi wananufaika na huduma mbali mbali za Mifuko ya Hifadhi
ya jamii”, alieleza.
Kw
a upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk Charles Kimei, alisema
azma yao ni kuhakikisha kuwa ushirikiano na wadau wanamkomboa kiuchumi
mwananchi hususan mwenye kipato cha
chini kwa kumpatia mkopo wenye riba ya asilimia 14 tu kwa mwaka.
Kuhusu marejesho alisema ni kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitano.
Ushirikiano
wetu na PSPF bado una muendeleo ulio
mpana kwani kwa pamoja tunadhamiria hapo baadae kuingiza sokono mikopo kwa
ajili ya wastaafu ‘pensioners’.
Alisema
mpango huu wa utoaji wa mikopo kw wastaafu una lengo la kuleta faraja na
kuwasaidia wastaafu katika kukidhi mahitaji yao mbali mbali ya kimaisha ikiwamo
kulipia gharama za matibabu, ada za shule za watoto au wajukuaa na kuendesha biashara ndogo ndogo
zitakazosaidia kupunguza ukali wa maisha ya kila siku.
Dk
Kimei alifafanua kuwa nia yao ni kujenga
mazingira mazuri kwa wastaafu walio wanachama wa PSPF ili kustaafu kusiogopwe
na kuonekana ni mwanzo wa kuanza kwa kipindi cha maisha ya shida yasiyokuwa
na matumaini.
“Tunataka
kujenga tabia ya kuwafanya wafanyakazi wanapopata barua za kustaafu
wasihuzunike kama ilivyozoeleka”, alidokeza.
Alisema
kuwa mwanachama wa PSPF anayetaka mkopo anatakiwa aende kwenye tawi lolote la
benki ya CRDB ililopo karibu naye ili kupata huduma.
Bw. Mayingu akitoa hotuba yake kuelezea ushirikiano huo ambao lengo lake kubwa ni kupanuan wigo wa huduma kwa Wanachama wa Mfuko huo.
Dkt. Charles Kimei, akitoa hotuba yake kueleza jinsi benki yake ilivyofurahishwa na ushirikiano huo.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, akitoa hotuba ya ukaribisho.
Mkurugenzi wa Mipango na Uwekezaji wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, (katikati), na Msaidizi Mtendaji wa Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Bw.Keneth Kasigila, wakimsikiliza Mkurugenzi wa Wateja wa Mashirika wa CRDB, Bw.Goodluck Nkini, (kushoto), wakati wa hafla hiyo.
Bw. Mayingu (kushoto) na Dkt. Kimei, wakibadilishana mawazo muda mfupi kabla ya kufanyika kwa uzinduzi huo.
Viongozi wa juu wa PSPF, wakipiga makofi wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya maafisa wa CRDB waliohudhuria hafla hiyo.
Baadhi ya maafisa wa PSPF.
Baloziwa PSPF, Mrisho Mpoto, (kushoto), akiongoza kuimba wimbo wa taifa.
Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles Kimei, (kushoto) na Balozi wa PSPF, Bw. Mrisho Mpoto (katikati), wakimsikiliza Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo.
Baadhi ya maafisa wa PSPF waliohudhuria hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mipangona Uwekezaji wa PSPF, Bw. Gabriel Silayo, akitoa neno la shukrani mwishoni mwa hafla hiyo.
Anna Lukando wa kampuni ya Ardhi Plan Limited, yenye ushirikiano na PSPF, akizungumzia jinsi wanachamawa Mfuko huo wanavyoweza kufaidika naupatikanajiwa viwanja vilivyopimwa kisheria.
Maafisa wa PSPF na CRDB wakifuatilia hafla hiyo.
Maafisa wa CRDB
|
Meneja wa Mpango wa Uchangiaji wa Hiari, (PSS), wa Mfuko wa Pensehni wa PSPF, Bi.Mwanjaa Sembe (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango huo, mfanyakazi wa CRDB, Bi. Fausta Urassa.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (kulia), akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), mfanyakazi wa CRDB, Bw.Alfred Kessy.
Balozi wa PSPF, Bw. Mrisho Mpoto, (kulia),akimkabidhi kadi ya kujiunga na mpango wa uchangiaji wa hiari (PSS), mfanyakazi wa CRDB, Bi. Flora Munisi.
|
Picha ya pamoja ya wanachama wapya wa PSPF na maafisa wa Mfuko huo akiwemo Balozi Mpoto.
|
Uzinduzi rasmi ukifanyika.
No comments:
Post a Comment