TANGAZO


Tuesday, February 28, 2017

SERIKALI KUFANIKISHA SOKA KUSHIRIKI OLIMPIKI TOKYO 2020

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau wa soka leo Jijini Dar es Salaam kuhusu namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki na kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 katika kikao cha  Wadau Tuzungumze kilichoandaliwa na Wizara. (Picha zote na  Shamim Nyaki – WHUSM)
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye akizungumza na wadau wa soka leo Jijini Dar es Salaam kuhusu namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki na kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 katika kikao cha  Wadau Tuzungumze kilichoandaliwa na Wizara.
Katibu Mkuu Wizara ya  Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof.Elisante Ole Gabriel  akieleza jambo kwa wadau wa Soka   (hawapo pichani)   kuhusu namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki na kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 leo Jijini Dar es Salaam katika kikao cha  Wadau Tuzungumze kilichoandaliwa na Wizara.
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw. Omary Singo  akitoa maelezo kuhusu mikakati ya Wizara katika kufanikisha timu ya soka  ya Tanzania  kushiriki Olimpiki Tokyo 2020 leo Jijini Dar es Salaam katika kikao cha  Wadau Tuzungumze kilichoandaliwa na Wizara.
Msemaji wa Shirikisho la Soka nchini (TFF) Bw. Alfred Lukas akichanhia mada wakati wa kikao cha kujadili namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki na kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 katika kikao cha Wadau Tuzungumze kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.  
Mjumbe wa Kamati ya Usuluhishi na Nidhamu kutoka Baraza la Michezo la Taifa  Bibi: Zainab Mbiro akitoa maoni yake kuhusu namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki na kushinda michezo ijayo ya Olimpiki Tokyo 2020 katika kikao cha Wadau Tuzungumze kilichoandaliwa na Wizara leo Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe Nape Moses Nnauye (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wadau wa soka nchini baada ya kumaliza kikao cha kujadili namna gani timu ya Soka ya Tanzania inaweza kushiriki na kushinda michezo ya Olimpiki Tokyo 2020 kilichofanyika leo Jijini Dar es Salaam.

Na Lorietha Laurence
WAZIRI wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye ametoa wito kwa wadau wa michezo nchini kushirikiana na Serikali kwa kupeleka michezo mbalimbali ikiwemo soka kwenye mashindano ya Olimpiki yanayotarajiwa kufanyika mjini Tokyo Japan mwaka 2020 ili kupata nafasi ya kushinda.

Ameyasema hayo leo Jijini Dar es Salaam  alipokutana na wadau wa soka katika muendelezo wa kipindi chake  cha “Wadau  Tuzungumze” lengo ikiwa ni kujadili namna ambavyo timu ya mpira wa miguu itakavyoweza kushiriki katika mashindano hayo ya Kimataifa.

Ameongeza kwa kusema kuwa ushiriki wa timu za mpira wa miguu kwenye mashindano ya  Olimpiki ni muhimu katika kukuza na kuendeleza soka huku akiwataka wadau hao kupeleka michezo mingi zaidi ili kupata nafasi ya kushinda medali mbalimbali.

“ Lengo  letu ni  kupata ushindi hivyo kwa kupeleka michezo mingi katika mashindano haya ya Olimpiki tunajitengenezea nafasi nzuri ya kurudi na ushindi  na kuondokana na dhana ya kuwa washiriki ” alisema Mhe.Nape.

Aidha aliwataka watanzania kushirikiana kwa pamoja katika kuhakikisha tunapata ushindi kwa kuwapa moyo wachezaji wetu ikiwemo uhamasishaji kupitia wadau mbalimbali wakiwemo wasanii wa muziki wa kisasa.

“Ushindi ni wetu sote hivyo ni wajibu wetu  kuweka juhudi za dhati katika kuhamasisha wachezaji  kwa kuwapa moyo ili waweze kurudi na ushindi na tayari nimeunda timu ya watu kumi kwa ajili ya kuhamasisha ushiriki wa Serengeti Boys katika mashindano ya AFCON Gabon” alisema Waziri Nape.

Kamati hiyo itakayoongozwa  na Charles Hillary itakuwa na wajumbe wengine ambao ni Selestine Mwesigwa,Beatrice Singano, Hassan Abbas, Ruge Mutahaba,Hoyce Temu,Eric Shigongo, Maulid Kitenge, Naseeb Abdul (Diamond) na Ally Kiba.

No comments:

Post a Comment