Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki akizungumza na watumishi wa ofisi yake juu ya safari ya kuhamia Dodoma iliyoanza rasmi leo kwa kuhamisha vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Laurean Ndumbaro wakiuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo, leo Jijini Dar es Salaam wakielekea Dodoma kwenye Makao Makuu ya nchi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki, Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Laurean Ndumbaro na Naibu Katibu wa Ofisi hiyo, Bi. Susan Mlawi wakifuatilia kwa makini uhamishwaji wa vifaa vya Ofisi yao kabala yakuondoka kwenda Dodoma leo hii.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah Kairuki na Katibu Mkuu wa Ofisi hiyo, Dkt. Laurean Ndumbaro wakiuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya ofisi vya kundi la kwanza la watumishi wa ofisi hiyo, leo Jijini Dar es Salaam wakielekea Dodoma kwenye Makao Makuu ya nchi.
Na Daudi Manongi-Maelezo.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa
Umma na Utawala Bora, Mhe. Angellah J. Kairuki amezindua rasmi safari ya awamu ya
kwanza kwa kuaga msafara wa magari yaliyobeba vifaa vya Ofisi vya kundi la
kwanza la watumishi wa ofisi hiyo kwenda
Dodoma.
Akizungumza katika uzinduzi huo, Mhe. Kairuki alisema umefika
wakati wafanyakazi wa Serikali kuanza safari ya kuhamia Makao Makuu Dodoma ili kutimiza
ahadi iliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli
wakati wa Maadhimisho ya kumbukumbu ya siku ya Mashujaa.
“Kufuatia agizo la Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Waziri Mkuu
kama kiongozi na mratibu wa shughuli za Serikali alihamia Dodoma Mwezi Septemba
2016, Wizara nyingine zimeendelea na maandalizi ya kutekeleza
azma hii ya Serikali, nami leo napenda kutumia fursa hii kuuarifu umma wa Watanzania
kuwa Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora imekamilisha
maandalizi ya kuhamia Dodoma na hivi punde vifaa vya kundi la kwanza vitaondoka
kwenda Dodoma”, aliongeza Mhe. Kairuki.
Amesema katika kundi la kwanza jumla ya watumishi 87
watahamia Dodoma na litahusisha uongozi wa Juu wa Wizara ukiwajumuisha Waziri wa
Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Katibu Mkuu
na Naibu Katibu Mkuu na baadhi ya Wakurugenzi, Wakurugenzi Wasaidizi, Maafisa Waandamizi
na watumishi wengine.
Katika hatua nyingine Mh. Kairuki alisema wale wote wanaohitaji
kukutana na Waziri, Katibu Mkuu na Naibu Katibu Mkuu wake wafike katika Ofisi zilizopo
Dodoma na kwa masuala yote yanayohusu Sera na Sheria za Utumishi wa Umma na Utawala
wa Utumishi wa Umma kwa ujumla yatatekelezwa Mjini Dodoma.
Aidha, masuala ya Mishahara, Uendelezaji rasilimaliwatu,
Ukuzaji maadili, Anuai za jamii, Uchambuzi, ushauri na Utendaji kazi na Huduma ya
teknolojia ya habari na mawasiliano, yataendelea kushughulikiwa na ofisi ya Dar
es Salaam.
Alisema Ofisi yake itafunguliwa rasmi
Mjini Dodoma, tarehe 30 Januari 2017 na itakuwa katika Jengo la College of
Humanities and Social Sciences katika eneo la Chuo Kikuu cha Dodoma kama makao yake
ya muda mpaka hapo itakavyoelezwa vinginevyo.
No comments:
Post a Comment