![]() |
Dkt. Juliana Palangyo |
Na Woinde Shizza, Arusha
WAKUU wa
mashirika umeme kutoka katika nchi kumi za Afrika zinazozalisha
umeme (Eastern Africa Power pool (EAPP), zimekutana jijini Arusha kwa malengo ya kujadili mfumo wa usafirishaji wa umeme ikiwa ni pamoja na namna wananchi wao watakavyoweza pata nishati ya umeme kwa uraisi tofautina sasa.
Hayo yalisemwa na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Dkt. Juliana Palangyo alipokuwa akizungumza katika ufunguzi wa mkutano wa wakuu wa mashirika ya umeme katika nchi hizo za eastern Africa power pool (eapp) mapema leo.
Palangyo alisema kuwa lengo halisi ni kuweza kujadili mambo mbalimbali yahusuyo nishati ya umeme kwa watumiaji wake kwani kuna
uwezekano mkubwa wa nchi zote zilizo kwenye umoja huo.
Alisema kwa sasa yapo baadhi ya makampuni ambayo yalikuwa yanauza
umeme kwa gharama kubwa hasa kwa wananchi ambao hawajapata huduma hiyo ya umeme lakini kupitia umoja huo wataweza kupata nishati hiyo kwa gharama
nafuu.
"Hizi nchi za eastern tumekutana hapa ili tujadili namna ambayo tunaayo wanayoweza kutafuta namna ya kuzalisha umeme kwa bei nafuu na kisha nchi hiyo itaweza kuuza umeme kwa bei ndogo"aliongeza
palangyo.
Hataivyo kwa upande kaimu meneja uhusiano wa Shirika la
Tanesco Leila Muhaji alisema kuwa katika mkutano huo
pia watajadili namna ambavyo Tanzania itajenga njia ya usafirishaji wa umeme wa njia ya maji ambayo itatoka nchi ya tanzania kwends kenya,zambia,pamoja na nchi nyingine Muhaji alisema kuwa tanzania itanufaika na ujenzi wa njia hizo hivyo
jamiii itanufaika kwa kiwango kikubwa sana kama ilivyo kwenye nchi ambazo zimeendelea duniani.
"Hataivyo mara baada ya huu mkutano wa wakuu wa nchi zinazolisha umeme tunatarajia pia kuwepo na wadau wengine ambao ni mawaziri kutoka nchi zote ambao nao sasa wataweza kuweka mambo sawa ili huduma iweze kumfikia mlengwa," aliongeza Muhaji.
Alimalizia kwa
kutaja nchi ambazo zina unda umoja huo kuwa ni Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Sudan, DR Congo, Ethiopia, Djbout,
Libya pamoja na Egypt.
No comments:
Post a Comment