TANGAZO


Tuesday, January 24, 2017

Viongozi waliopora nchi zao mamilioni ya pesa wakiwa madarakani

JammehHaki miliki ya pichaREUTERS
Image captionYahya Jammeh
Zaidi ya dola milioni 11 zinaripotiwa kutoweka kutoka kwa hazina ya taifa nchini Gambia, kufuatia kuondoka kwa kiongozi wa muda mrefu Yahya Jammeh.
Jammeh alikwamia madaraka kwa karibu miezi miwili licha ya kushindwa kwenye uchaguzi wa urais mwezi Disemba.
Bwana Jammeh ambaye kwa sasa yuko nchini Equatorial Guinea, si kiongozi wa kwanza anayelaumiwa kwa kupora pesa za umma. Kuna wale walipora nyingi zaidi na hawa ni baadhi yao.
Sani Abacha, Nigeria
AbachaHaki miliki ya pichaAFP
Image captionSani Abacha
Sani Abacha, kiongozi wa Nigeria kutoka mwaka 1993 hadi 1998, aliripotiwa kupora kati ya dola bilioni moja na bilioni 5 kutoka kwa hazina ya taifa. Mwaka 2014 idara ya haki nchini Marekani ilisema kuwa ilitwaa mali ya Abacha yaliyokuwa yameibwa ya thamani ya dola milioni 450.
Suharto, Indonesia
SuhartoHaki miliki ya pichaAFP
Image captionSuharto
Suharto, rais wa Indonesia kutoka mwaka 1967 hadi mwaka 1998, anadaiwa kuisafisha hazina ya taifa ya nchi kwa hadi dola bilioni 35. Mwaka 2000 aliwekwa chini ya kuzuizi cha nyumbani na kushtakiwa kwa kuiba dola milioni 570. Lakini madaktari waligundu kuwa alikuwa mgonja sana kuweza kufika mahakamani . Aliaga dunia mwaka 2000 .
Mobutu Sese Seko, Zaire
ZAIRE PRESIDENT
Image captionMobutu Sess Seko
Kiongozi wa Zaire ambayo sasa ni Jamhuri ya Demokrasi ya Congo kutoka mwaka 1965 hadi mwaka 1997, Mobutu aliongoza utawala dhalimu ambao ulikandamiza upinzani. Pia aliishi maisha ya anasa na kujirundikia mali nyingi ikiwemo nyuma ya viumba 30 huko Lausanne ya thamani ya dola milioni 5.5. Anakisiwa kuiba dola bilioni 5.
Ferdinand Marcos, Ufilipino
MarcosHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionFerdinand Marcos
Mke wa Marcos, Imelda alikuwa na viatu 3000. Marcos anaaminiwa kuiba dola bilioni 10 akiwa madarakani kati ya mwaka 1965 na 1986. Baada ya kifo chake kesi kadha ziliilazimisha Uswizi ambapo alificha pesa hizo kurudisha karibu dola milioni 7000 kwa utawala wa Ufilipino.
Ali Abdullah Saleh, Yemen
SalehHaki miliki ya pichaAFP
Image captionAli Abdullah Saleh
Rais wa zamani wa Yemen Ali Abdullah Saleh anakisiwa kupora karibu dola milioni 60 wakati akiwa ofisini. Aliondolewa madarakani mwaka 2012 wakati wa mapinduzi ya nchi za kiarabu lakini sasa anashirikiana na waasi wa Houthi katika nchi hiyo iliyokumbwa na mapigano.
Slobodan Milosevic, Serbia
MilosevicHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSlobodan Milosevic
Slobodan Milosevic, Ni kiongozi dhalimu ambaye aliitawala Serbia kati ya mwaka 1989 na 1997. Alishtakiwa kwanza kwa kuendesha mauaji ya halaiki. Lakini pia alishtakiwa kwa kupora pesa za umma. Kiwango alichopora hakijulikani lakini anakisiwa kuiba kati ya dola bilioni 1 na bilioni 4. Aliaga dunia mwaka 2006 akiwa kwenye mahakama ya Hague.
Hosni Mubarak, Misri
MubarakHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionHosni Mubarak
Alipinduliwa mwaka 2011. Hosni mubarak alishtakiwa kwa kuiba pesa zilizonuiwa kukarabati ikulu za rais na kuzitumia kujenga miradi yake binafsi. Mubarak na wanawe wa kiume walipatikana na hatia ya kuiba zaidi ya milioni dola 17 kati kipindi cha miaka minane. Alihukumiwa kifungi cha miaka mitatu jela huku wanawe wakihukumiwa kifungo cha miaka minne kila mmoja.
Ben Ali, Tunisia
Ben AliHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBen Ali
Mwaka 2011 wakati wa kupinduliwa kwa Ben Ali, yalianza mapinduzi ya nchi za kiarabu. Ali na mkewe walikimbia kwenda Saudi Arabia lakini mahakama ya Tunisia iliwahukumu bila ya wao kuwepo kifungo cha miaka 35 jela kwa kupora pesa za umma. Wakati wa kesi yao mwendesha mashataka alisema kuwa vito vya thamani ya dola milioni 27 na pesa vilipatikana ndani ya moja ya nyum

No comments:

Post a Comment