Serikali ya Marekani imeidhinisha mpango wa kuliuzia jeshi la Kenya ndege 14 za kijeshi zenye thamani ya dola milioni 418, Idara ya ulinzi nchini humo imetangaza.
Ndege hizo zitatumika katika vita dhidi ya wapiganaji wa al-Shabab wenye makao yao huko nchini Somalia ambao wamefanya mashambulizi mabaya zaidi nchini Kenya, idara hiyo imeongezea.
Imesema kuwa ndege hizo kwa jina Air Tractor zitaweza kukabiliana na wapiganaji hao kwa karibu ikilinganishwa na ndege za sasa za f-5 fleet.
Mauzo hayo yanachangia sera ya kigeni ya usalama ya taifa la Marekani kwa kuwa Kenya inaongoza katika eneo hilo katika vita dhidi ya wapiganaji hao.
No comments:
Post a Comment