Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Magufuli akiwasili katika kituo cha mabasi yaendayo haraka
Kariakoo Gerezani alipoenda kuzindua Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo
haraka jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni Makamu wa Rais wa Benki ya Diunia kwa
Ukanda wa Afrika Maktahar Diop.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka
Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa
Makame Mbarawa akifafanua jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na
Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI, George
Boniphace Simbachawene akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza
leo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia
Kanda ya Afrika Makthar Diop akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza
leo jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda
akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi
yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na
Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga akimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga (aliyesimama) wakati wa
hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es
Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli akiwaongoza viongozi na wananchi wa Dar es Salaam
kuimba wimbo wa taifa wakati wa hafla ya uzinduzi Miundombinu na Huduma za Mabasi
yaendayo haraka jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Mbunge wa Ilala Mussa
Zungu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhan Madabida,Waziri wa OR –
TAMISEMI George Simbachawene, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika
Makthar Diop, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa,
Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Augustine Mahiga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Paul Makonda.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam
wakifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi wakati wa hafla ya uzinduzi wa
Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka awamu ya kwanza leo jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli akitazama jiwe la msingi mara baada ya kuzindua
rasmi Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka awamu ya kwanza leo
jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia kwa Rais ni Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI
George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame
Mbarawa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia), akiwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe
(katikati) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop wakimwagilia
maji mti uliopandwa kama kumbukumbu za uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za
mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli akipeana mkono na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia
Kanda ya Afrika Makthar Diop wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na
Huduma za mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar
es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli akieenda kumtumza msaani wa muziki Mrisho Mpoto na
Banana Zoro wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo
haraka jijini Dar es Salaam leo. Uzinduzi huo umefanyika katika kituo cha
mabasi yaendayo haraka cha Gerezani Kariakoo amba Mpoto na Banana waklitumbuiza
wimbo wao unaohamasisha wananchi kufanya kazi hali iliyomvutia Rais Magufuli.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa
kiserikali na siasa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za
mabasi yaendayo haraka, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam. Aliyemshikana
naye mkono ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa kiserikali na siasa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Pombe Joseph Magufuli akiendesha Basi la Mwendokasi mara baada ya kuzindua
Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka, awamu ya kwanza leo jijini Dar
es Salaam.
Baadhi ya wanacnhi wakiwa katita mageti ya
kuingilia katika Kituo cha Mabsi yaendayo haraka cha Gerezani Kariakoo
walipokuwa wakimshuhudia Rais Magufuli akiendesha Basi kama ishara ya kuzindua
Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka leo jijini Dar es Salaam.
Na DaudiManongi-Maelezo.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt.John Pombe Magufuli ameagiza kujengwa kituo kikubwa cha kupaki magari na kituo cha dala dala ili kuwawezesha wananchi wanaotumia magari binafsi kupaki Kimara mwisho na kutumia usafiri wa mwendokasi ili kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.
Rais Magufuli ametoa wito huo, leo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji wa Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka (BRT), katika Kituo Kikuu cha Mabasi kilichopo Kariakoo eneo la Gerezani.
“Wito wangu ni kwamba kuna watu wengi wana magari madogo madogo na wanatoka sehemu mbalimbali mpaka kufika kituo cha Kimara mwisho na kuna eneo kubwa pale la hifadhi ya barabara ambalo halihitaji hata kulipa fidia ili kulitumia, wananchi wanaona adha ya foleni iliyopo lakini hawana sehemu ya kupaki magari yao, ili watumie magari ya mwendo kasi, nawaomba mjenge kituo cha magari madogo madogo eneo hili la Kimara ili wananchi hawa wafaidike vyema na mradi huu”, aliongeza Rais Magufuli.
Aidha, Rais Magufuli ametoa wito kujengwa kwa kituo cha mabasi ya daladala katika eneo la Kimara mwisho ili kuwasaidia wananchi wanaofika katika kituo cha magari ya mwendo kasi kutopata shida ya kuunganisha magari ya kwenda Mbezi na sehemu nyingine za Jiji kwani watakuwa na kituo rasmi.
Awali akizungumzia mradi huo, Rais Magufuli alisema kuwa iliwachukua abiria kusafiri kwa zaidi ya masaa matatu kutoka Kimara mpaka Posta lakini kukamilika kwa mradi huu kumesaidia kurahisisha abiria kufika kituo cha Posta kwa kutumia dakika 30 mpaka 40 na hivyo mradi huu kuwa kichocheo kikubwa cha uchumi katika maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es Salaam.
Alisema kuwa kukamilika kwa mradi huu wa awamu ya kwanza wenye kilometa 20.9, umetumia jumla ya shilingi bilioni 403.5, ambapo Tanzania imechangia bilioni 86.5 na Benki ya Dunia wametukopesha sh. bilioni 317.
Amesema kuwa kukamilika kwa awamu ya kwanza kume kuwa chachu ya kuanza kwa awamu ya pili ambayo itajengwa kuanzia Gerezani mpaka Mbagala, ambapo mpaka kufikia awamu ya sita kutalifanya Jiji la Dar es Salaam kuwa la kisasa na salama zaidi na hivyo kuwa Jiji kuu la Biashara.
Rais Magufuli amewataka Watanzania kutumia vyema miundombinu ya mabasi yaendayo haraka na pia madereva wa magari madogo kuzingatia sheria kwa kutotumia njia hizo.
Rais Magufuli ametoa shukrani kwa Benki ya Dunia kwa ushirikiano wao mkubwa katika kufanikisha mradi huo na miradi mingine nchini na kuwataka kusaidia katika kufanikisha mradi wa kujengwa kwa barabara za juu katika eneo la Ubungo na wale wote wanaohusika katika kupata mkandarasi wafanikishe haraka suala hilo, ili kusaidia mabasi yaendayo haraka kupita kwa urahisi na hivyo kutimiza dhana halisi ya mabasi hayo.
No comments:
Post a Comment