Rais mpya wa Gambia Adama Barrow amemteua mwanamke mwenye ushawishi mkubwa ambaye aliwahi kuwa mshirika wa aliyekuwa rais wa taifa hilo Yahya Jammeh kabla ya kujiunga na upinzani ulioshinda uchaguzi kuwa makamu wake wa urais.
Aidha mwanamke huyo kwa jina Fatoumata Jallow-Tambajang alimtishia kiongozi huyo kwa kumfungulia mashtaka.
Lakini watu wanatilia shaka iwapo bi Tambajang mwenye umri wa miaka 68 anahitimu kupewa wadhfa huo kutokana na umri wake.
- Barrow: "Hii ni Gambia mpya"
- Buhari kuongoza mazungumzo kuhusu Gambia
- Mawaziri watatu zaidi wajiuzulu Gambia
- Yahya Jammeh awasili Equatorial Guinea
Bi Tambajang aliwahi kuhudumu kama waziri wa afya na maswala ya kijamii wakati wa utawala wa Yahya Jammeh lakini akalazimika kwenda mafichoni baada ya kukosana naye.
Baadaye alikuwa kiungo muhimu katika kuanzisha upinzani uliomshinda Jammeh mnamo tarehe mosi mwezi Disemba, na alikuwa wa kwanza kumtishia kwamba atamfunguliwa mashtaka kwa uhalifu aliotekeleza wakati wa utawala wake, wito unaoenda kinyume na rais Adama Barrow.
Bw Jammeh alienda mafichoni siku ya Jumamosi baada ya shinikizo kutoka kwa viongozi wa kieneo huku jeshi la Senegal likiingia nchini humo na kutishia kumkamata.
No comments:
Post a Comment