Kiongozi wa upinzani nchini DR Congo Etienne Tshisekedi ameelekea nchini Ubelgiji kwa matibabu ya kiafya kulingana na chombo cha habari cha AFP.
Chombo hicho cha habari kimeongezea kuwa hatua hiyo inajiri wakati ambapo chama chake kinaendelea na mazungumzo ya kugawana mamlaka kufuatia hatua ya rais Laurent Kabila kukataa kujiuzulu baada ya muda wake wa kuhudumu kukamilika mwezi uliopita.
Viongozi wa kanisa la Katoliki nchini humo walifanikiwa kuweka makubaliano ambapo bwana Tshisekedi alitarajiwa kupewa wadhfa wa serikali ya mpito hadi pale uchaguzi utakapofanyika mwishoni mwa mwaka huu.
No comments:
Post a Comment