TANGAZO


Tuesday, January 24, 2017

MAKAMU WA RAIS WA BENKI YA DUNIA KANDA YA AFRIKA AWASILI KUSHIRIKI UZINDUZI WA MABASI YA MWENDO KASI-BRT

Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiwa na Mgeni wake ambaye ni Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, wakiwa katika chumba cha kupumzikia wageni maalumu katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Jijini Dar es salaam. Kulia ni Mwakilishi Mkazi wa Benki ya Dunia katika nchi za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi Bi. Bella Bird. (Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini-WFM)
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, (wa pili kulia aliyeshika dafu) alipowasili nchini, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (wa tatu kushoto) ambapo anatarajiwa kushiriki katika uzinduzi wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017, na baadaye kufanya mazungunzo na Waziri huyo alasiri. 
Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika Bw. Makhtar Diop, (kulia) akipoza koo kwa kupata dafu alipowasili nchini, akiwa na mwenyeji wake Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango (kulia) ambapo anatarajiwa kuungana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, katika uzinduzi wa Mradi wa mabasi yaendayo haraka BRT, Januari 25, 2017. 
Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, Mhe. Dkt. Philip Mpango, akiteta jambo na Mkurugenzi Mkazi, baada ya mapokezi ya Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop. 
Benny Mwaipaja, WFM, Dar es salaam
24. Januari 2017
MAKAMU wa Rais wa Benki ya Dunia anayeshughulikia masuala ya Kanda ya Afrika, Bw. Makhtar Diop, amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku tatu ambapo pamoja na mambo mengine, anatarajia kushiriki uzinduzi wa Mradi wa Mabasi yaendayo haraka tukio linalotarajiwa kufanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Jijini Dar es salama kesho asubuhi.

Makamu huyo wa Rais wa Benki ya Dunia,  amelakiwa na Mwenyeji wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango kati Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere pamoja na Mkurugenzi Mkazi wa Benki hiyo anayehudumu katika Nchi za Tanzania, Burundi, Somalia na Malawi, Bibi Bella Bird.
Akiwa nchini, Bw. Diop atakutana na kufanya mazungumzo pia Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango,  Gavana wa Benki Kuu Benno Ndulu, Sekta Binafsi ambapo mazungumzo yao yanatarajiwa kujikita katika Miradi kadhaa ya maendeleo inayofadhiliwa ama kugharamiwa na Benki hiyo kwa njia ya ruzuku na mikopo yenye masharti nafuu ambayo mpaka sasa inakadiriwa kufikia thamani ya Dola Bilioni 4 nukta 7.

No comments:

Post a Comment