TANGAZO


Saturday, January 21, 2017

MAADHIMISHO YA MWAKA MPYA WA KICHINA, MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU: UHUSIANO WA TANZANIA NA CHINA UNACHOCHEA UCHUMI

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akisalimiana na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye mara baada ya kuwasili katika viwanja vya mnazi mmoja kwa ajili ya kufungua sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Jamhuri ya watu wa China leo jijini Dar es Salaam. Katikati ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Charles Mwijage na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga. (Picha zote na Frank shija & Shamimu Nyaki)
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akihutubia mamia ya wakazi wa Jiji la Dar es Salaam leo wakati hafla ya kufungua sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa Jamhuri ya watu wa China.China inasherehekea Mwaka Mpya ambapo mwaka huu umepewa jina la Jogoo (Rooster). 
Balozi wa China nchini Tanzania Balozi Dkt. Lu Youqing akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan (wapili kutoka kulia) akiwaongoza viongozi na wananchi wakati wa kuimbwa wimbo wa Taifa katika hafla ya maadhimisho ya waka mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nape Moses Nnauye, Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akimsikiliza kwa makini Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya vikundi mbalimbali vya burudani kupitia Sanaa wakionyesha umahiri wao wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya vikundi mbalimbali vya burudani kupitia Sanaa wakionyesha umahiri wao wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. 
Kijana wa Kichina akitoa burudani ya sarakasi wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. 
Vijana wa Kichina wakitoa burudani ya sarakasi wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. 
Vijana wa Kitanzania wakitoa burudani ya Kung Fu wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa hundi ya shilingi milioni 70 na laki nne kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Chato kutoka kwa Balozi wa China nchini Dkt. Lu Youqing wakati wa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakifuatilia mambo mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea katika hafla ya kuadhimisha mwaka mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. 
Baadhi ya washiriki wa maadhimisho hayo wakitembelea baadhi ya mabanda yaliyopo katika viwanja vya Mnazi Mmoja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho yam waka mpya wa China leo jijini Dar es Salaam. China wanasherehekea mwaka mpya leo na kesho katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 11 jioni. 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa Serikali ya Tanzania na Balozi wa China hapa nchini Dkt. Lu Youqing baada ya kumalizika kwa hafla ya uzinduzi wa sherehe za maadhimisho ya Mwaka Mpya wa China leo jijini Dar es Salaam.Maadhimisho hayo yanafanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja kuanzia saa 4;00 asubuhi hadi saa 11 jioni na yanatarajiwa kumalizika kesho tarehe 22 Januari 2017.

Na Jacquiline Mrisho - Maelezo
UHUSIANO uliopo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya watu wa china ni kichocheo kikubwa cha maendeleo baina ya pande zote mbili.

Kauli hiyo imetolewa leo na Makamu wa Rais, Mhe. Samia Suluhu Hassan wakati wa sherehe za maadhimisho  ya mwaka mpya wa Kichina zilizofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mhe. Samia amesema kuwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatambua umuhimu wa ushirikiano huo na ameipongeza Serikali ya China kwa kuwa mshirika muhimu katika kusaidia utekelezaji wa miradi mbalimbali nchini.

Miradi hiyo inayotekelezwa na Serikali ya Jamhuri ya watu wa China inajumuisha Sekta za Elimu, Afya, Kilimo Ujenzi na Uchukuzi.

“Ushirikiano uliopo kati ya nchi yetu na China utawezesha Tanzania kujenga viwanda ambavyo vitasaidia kukuza uchumi wa nchi na kuongeza pato la taifa,” alisema Mhe. Samia.

Kwa upande wake Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa dhamira yake ya dhati ya kuwaletea maendeleo Watanzania pamoja na kupambana na rushwa.  

Dkt. Lu Youqing amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Serikali ya China itaendelea kushirikiana na Tanzania kama ilivyoasisiwa na waasisi wa mataifa hayo.

Ni desturi kwa taifa la China kuadhimisha mwaka mpya na kuupa majina tofauti kulingana na miaka, mwaka huu wa kichina unaitwa ‘mwaka wa Kuku Jogoo’ ambao hutokea kila baada ya miaka 60.


Sherehe hizo zilihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali akiwemo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Dkt. Augustine Mahiga, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Aziz Mlima, Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe.Charles Mwijage, jamii ya wachina waliopo Tanzania. 

No comments:

Post a Comment