TANGAZO


Wednesday, January 25, 2017

Bana Alabed: Msichana wa Syria amwandikia barua Donald Trump

Bana Alabed, 7Haki miliki ya pichaAFP
Image captionBana, kwa sasa anaishi Uturuki
Bana Alabed, msichana wa miaka saba kutoka Aleppo ambaye alipata umaarufu duniani kutokana na ujumbe ambao alikuwa akiandika kutoka Aleppo, amemwandikia Rais Donald Trump barua ya wazi.
"Lazima uchukue hatua kuhusu watoto wa Syria kwani ni sawa na watoto wako mwenyewe na wanahitaji amani kama wewe mwenyewe," ameandika.
"Nikiwa Aleppo sikuweza kucheza. Aleppo ulikuwa mji wa mauti."
Bana alifanikiwa kuondoka Aleppo pamoja na familia yake Desemba wakati wa mpango mkubwa wa kuwaondoa raia maeneo yaliyodhibitiwa na waasi.
Kwa sasa anaishi Uturuki.
Ukurasa wake wa Twitter ulipata umaarufu sana kutokana na ujumbe alioandika akiwa maeneo ya mashariki mwa Aleppo wakati maeneo hayo yalikuwa yamezingirwa na wanajeshi wa serikali.
Mamake, Fatemah - ambaye amekuwa akimsaidia kuandika ujumbe kwenye ukurasa huo wake - ametuma nakala ya barua hiyo kwa BBC.
Anasema Bana aliandika barua hiyo siku kadha kabla ya Trump kuapishwa kuwa rais, kwa sabbau alikuwa "anamuona Trump mara nyingi kwenye runinga.
@AlabedBanaHaki miliki ya pichaTWITTER / ALABEDBANA
Image captionTangu alipowasili Uturuki, Bana amekuwa akitumia ukurasa wake kuitisha kusitishwa kwa mapigano
Uturuki, nchi ambayo Bana anaishi kwa sasa, inaunga mkono upinzani nchini Syria.
Lakini msimamo wa Bw Trump bado haujulikani.
Rais huyo wa Marekani ameeleza nia yake ya kutaka kuwa na uhusiano mzuri na Urusi, na ameonekana kufurahishwa na Rais Vladimir Putin - anayemuunga mkono Rais wa Syria Bashar al-Assad.

No comments:

Post a Comment