Mtu mmoja mwenye umri wa miaka 70 kutoka eneo la Kansas nchini Marekani amekiri kushiriki katika wizi wa benki siku ya Jumanne akisema alifanya makusudi ili kumtoroka mkewe.
Lawrence Ripple aliiba katika benki moja ya mji wa Kansas mwezi Septemba na baadaye akajisalimisha kwa maafisa wa polisi.
Amewaambia wachunguzi kwamba ni heri kwenda jela badala ya kuishi nyumbani na sasa anakabiliwa na takriban miaka 20 Jela.
Mkewe aliandamana naye hadi mahakamani, lakini hajatoa tamko lolote kulingana na gazeti la The Star mjini humo.
Bwana Riple alimpatia ilani karani mmoja wa benki akitaka fedha na kumtishia kwamba ana bunduki kulingana na nakala za mahakamani.
Alipewa takriban dola 3,000 lakini hakwenda kokote.
Bado akiwa ndani ya benki hiyo alisimama akachukua kiti na kumwambia mlinzi kwamba yeye ndio mtu aliyekuwa akimtafuta.
Bwana Ripple alikuwa amechagua benki ilio na kituo cha polisi.
Taarifa ya polisi ilisema kuwa Ripple alikosana na mkewe mapema siku hiyo.
No comments:
Post a Comment