TANGAZO


Sunday, January 22, 2017

Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh amewasili Equatorial Guinea

Bwana Jammeh, aliaminiwa kusafiri kwenda GuineaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionBwana Jammeh, aliaminiwa kusafiri kwenda Guinea
Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh amewasili nchini Equatorial Guinea, siku moja baada ya kuachia madaraka kwa Adama Barrow, aliyemshinda katika uchaguzi wa urais mwezi Disemba mwaka jana.
Jammeh alisafiri kwa ndege kutoka Banjul hadi Guinea na baadaye kuendelea na safari yake kwenda Equatorial Guinea.
Hapo jana Bwana Jammeh alitangaza kwamba atang'atuka baada kuongozi Gambia kwa miaka 22.
Kwa mujibu wa jumuiya ya kiuchumi ya Afrika magharibi ECOWAS, Jammeh amewasili nchini Guinea. Siku ya Alhamisi ECOWAS illituma vikosi vyake nchini Gambia kumshurutisha Bwana Jammeh kukubali Adama Barrow aapishwe.
Jumuiya hiyo inasema imesitisha oparesheni yake ya kijeshi Gambia lakini wanajeshi elfu saba watasalia nchini humo kudumisha usalama, huku Adama Barrow akitarajiwa kurejea Gambia kutoka nchi jirani ya Senegal muda mfupi ujao.
Yaya Jammeh akiwapungia mkono watu alipokuwa akiabiri ndege BanjulHaki miliki ya pichaAFP
Image captionYaya Jammeh akiwapungia mkono watu alipokuwa akiabiri ndege Banjul

No comments:

Post a Comment