TANGAZO


Friday, December 30, 2016

Nkurunziza aashiria kuwania muhula wa nne Burundi

Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Image captionRais wa Burundi Pierre Nkurunziza
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza amesema kuwa huenda akawania muhula mwengine iwapo katiba itabadilishwa ili kumruhusu kufanya hivyo.
Uamuzi wake wa kuwania muhula wa tatu mwaka uliopita ulizua ghasia ambazo zimesababisha mauaji ya zaidi ya watu 100.a
Wakati huo Nkurunziza alikuwa amenukuliwa akisema kuwa atajiuzulu mwaka 2020.
Hatahivyo siku ya Ijumaa rais huyo alitangaza kuwa hatowasaliti raia wake iwapo watamtaka kuwania kwa muhula mwengine wa nne.
Ameongezea kwamba mihula ya kuwania urais inaangaziwa sana siku za hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment