Ukaguzi wa maabara wa magunia ya mchele uliokamatwa na maafisa wa halmashauri ya kutoza ushuru nchini Nigeria unaoyesha kuwa mchele huo ni 'mchafu' na sio wa 'plastiki ' kulingana na shiirika la chakula na dawa nchini humo NAFDAC.
''Mchele huo una bakteria wengi zaidi'', alisema afisa wa Nafdac.
Madai ya maafisa wa shirika la kutoza ushuru nchini humo kwamba mchele huo uliokamatwa mjini Lagos wiki iliopita ulikuwa wa plastiki yalizua utata.
Hatahivyo wizara ya afya iliingilia kati na kusema kuwa hakuna ushahidi wowote kuhusiana na madai hayo.
''Violezo vya mchele huo vilivyopimwa vimebaini kwamba haufai kutumiwa kwa mahitaji ya kibinaadamu, viwango ambavyo vinapita idadi ya bakteria wanohitajika'',alisema afisa wa Nafdac.
Shirika la kutoza ushuru nchini humo likizungumza katika mkutano huohuo na vyombo vya habari limebaini kwamba kuna habari kwamba mchele mwingi ulifaa kuingizwa nchini humo kutoka mashariki hadi Afrika.
No comments:
Post a Comment