Mkurugenzi Muendeshaji wa Kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging Limited Bw. Joseph Wasonga akimpatia maelezo Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru kuhusu hatua iliyofikiwa kabla ya kiwanda hicho kalba hakijaanza kufanya kazi na kuzalisha vifungashio.
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Bi. Asumpta Mshana akiongea wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging Limited kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani na kumshukuru muwekezaji wa kiwanda hicho kwa kuamua kuwekeza katika mkoa wa pwani kwani itaisaidia kuongeza mapato katika mkoa na kuongeza ajira kwa wakazi.
Mkurugenzi Muendeshaji wa Kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging Limited Bw. Joseph Wasonga akiongea wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda hicho na kuishukuru Serikali kupitia taasisi zake ikiwemo NDC, NEMC,TBS na Ofisi ya Mkoa wa Pwani kwa ushirkiano walioupata wakati wa mchakato wa uanzishaji wa Kiwanda hicho hadi hapo kilipofika na kuzitaka taasisi za fedha nchini kuendelea kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa ajili ya kuwaaidia wawekezaji wazawa.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru akiongea wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging Limited kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani ambapo alimpongeza muwekezaji wa kiwanda hicho na kutoa rai kwa wakuu wa wilaya na mikoa nchini kuweka mazingira mazuri kwa ajili ya wawekezaji ikiwemo kutenga maeneo maalum kwa ajili ya viwanda kama ilivyo katika mkoa wa Pwani.
Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru (katikati), akikata utepe kuashirika uwekaji wa jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha Global Packaging kilichopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani, wakwanza kushoto ni Mkurugenzi Muendeshaji wa Kiwanda hicho Bw. Joseph Wasonga, watatu kutoka kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi Mkucha akifuatiwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi. Asumpta Mshana.
Katibu
Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt.Adelhelm Meru (katikati
mwenye miwani), Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) Mlingi
Mkucha (mwenye tai nyekundu), Mkurugenzi Muendeshaji wa Kiwanda cha vifungashio
Bw. Joseph Wasonga (wanne kutoka kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi. Asumpta
Mshana wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kiwanda hicho na
wafanyakazi wa NDC.
Na Hassan Silayo-Maelezo
WAKUU wa Mikoa na Wilaya nchini wametakiwa kuweka kuweka mazingira wezeshi kwa
wawekezaji nchini ikiwemo kutenga maeneo maalum kwa ajili ya ujenzi wa viwanda
nchini.
Akizungumza
wakati wa uwekaji jiwe la msingi katika kiwanda cha kutengeneza vifungashio
kilichopo wilayani Kihaba mkoani Pwani Katibu Mkuu Wizara ya Viwanda, Biashara
na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru amesema kuwa tukiwa tunaelekea katika nchi ya
viwanda serikali inajukumu la kutoa ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji nchini.
Dkt.
Adelhelm amesema kuwa viongozi hao hawana budi kuiga mfano wa Mkuu wa Mkoa wa
Pwani na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha kwa ushirikiano wanaoutoa kwa wawekezaji
ikiwemo kutenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda katika mkoa huo.
“Dhumuni
la serikali kwa sasa ni kuhakikisha tunaifikia nchi ya uchumi wa kati kupitia
viwanda,na hili tutalitekeleza pia kwa kushirikiana na sekta binafsi na ni
jukumu la viongozi ikiwemo wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa nchini kote kutoa
ushirikiano wa kutosha kwa wawekezaji ikiwemo kutenga maeneo kwa ajili ya
ujenzi wa viwanda”. Alisema Dkt. Adelhelm
Dkt.
Adelhelm aliongeza kuwa mpaka ifikapo mwaka 2020 Serikali imepanga kuhakikisha
sekta ya viwanda nchini inachangia asilimia 15 kwenye pato la taifa kutoka
asilimia 7.3 iliyopo hivi sasa.
Pia
Dkt. Adelhelm alisema kuwa Serikali imepanga kuongeza idadi ya ajira za
viwandani na ajira zitokanazo na sekta ya viwanda hadi kufikia asilimia 40
ifikapo mwaka 2020.
Naye
Mtendaji Mkuu wa Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC) Bw. Mlingi Mkucha amesema
kuwa shirika hilo litaendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji wote wenye nia
ya kuwekeza katika viwanda ikiwemo kupitia maandiko ya miradi yao na
kuwasimamia ili kuhakikisha kwa pamoja wanatimiza lengo la serikali ya awamu ya
tano ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
Bw.
Mkucha aliongeza kuwa katika wilaya ya Kibaha kuna hekari 330 zilizotengwa kwa
ajili ya viwanda vya aina mbalimbali ikiwamo viwanda vya kuunganisha magari,
vuwanda vya madawa na viwanda vya nguo hivyo kama kuna muwekezaji mwenye nia ya
kuwekeza katika sekta hizo aende katika ofisi za Shirika hilo ili kuweza
kujadili namna ya kutekeleza suala hilo.
Naye
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha Bi. Asumpta Mshana alisema kuwa ujenzi wa kiwanda
hicho katika mkoa wa pwani ni mwendelezo wa jitihada za kumuunga mkono Rais
Magufuli ya kufikia uchumi wa kati kupitia viwanda.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kiwanda cha kutengeneza vifungashio cha
Global Packaging Bw. Joseph Wasonga alishukuru jitihada za serikali na taasisi
zake kwa ushirikiano wanaoupata tangu wakiwa na wazo la kuanzisha kiwanda hicho
hadi kufikia hatua hiyo ya uzinduzi.
Bw.
Wasonga aliongeza kuwa dhumuni la kiwanda hicho ni kuzalisha vifungashio
milioni 16 hadi milioni 20 kwa mwaka na kuongeza zaidi idadi ya ajira kwa wakazi
wa maeneo yanayozunguka kiwanda hicho na maeneo ya jirani.
Kiwanda
cha hicho kinamilikiwa kwa ubia kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa(NDC) na
kampuni ya Wande Printing and Packaging inayomilikiwa na mzawa.







No comments:
Post a Comment