Pages

Tuesday, November 8, 2016

BALOZI SEIF IDDI AONGOZA MAZIKO YA ALIYEKUWA NAIBU KATIBU MKUU WA CCM ZANZIBAR, SALEH RAMADHAN FEROUZ

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akimfariji na kumpa pole mke wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar ambye pia ni Naibu Katibu Mkuu mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar Ndg. Saleh Ramadhan Ferouz, aliyefariki dunia Jumatatu kutokana na kuumwa maradhi ya tezi dume. 
Waumini wa dini ya Kiislamu wakiongozwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi, Makamu wa Rais mtaafu wa Serikali ya Muungano, Dk. Mohamedd Gharib Bilal pamoja na Viongozi wengine wa kisiasa na Serikali wakimsalia marehemu Saleh Ramadhan Ferouz katika Msikiti wa Ijumaa wa Kiembe Samaki. 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi, akitia mchanga katika kaburi la aliyekuwa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, maheremu Saleh Ferouz aliyezikwa katika Makaburi ya Mwanakwerekwe nje kidogo ya Mji wa Zanzibar leo. 
Makamu wa Rais mstaafu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Mohamed Gharib Bilal akitia mchanga katika kaburi la marehemu Saleh Ramadhan Ferouz hapo Mwanakwerekwe. 
Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai akitia mchanga katika kaburi la mtangulizi wake katika nafasi hiyo ya chama, marehemu Saleh Ramadhan Ferouz katika Makaburi ya Mwanakwerekwe.(Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)

No comments:

Post a Comment