Pages

Tuesday, November 8, 2016

BALOZI SEIF IDDI ATOA POLE KWA MSIBA WA MWENYEKITI MSTAAFU WA TUME YA UCHAGUZI ZANZIBAR JAJI ZUBEIR JUMA MZEE

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi akikabidhi ubani wa Serikali kwa Mzee Khamis Vuai (kulia), mwakilishi wa Familia ya Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), marehemu Jaji Zubeir Juma Mzee, aliyefariki dunia jana na kuzikwa kijiji kwao, Mbuzini, Wilaya ya Magharibi “A”.  
Baadhi ya wanafamilia ya Mwenyekiti mstaafu wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar, marehemu Jaji Zubeir Juma Mzee, wakipokea nasaha za pole kutoka kwa Balozi Seif (hayupo pichani), alipofika kutoa mkono wa pole. 
Wanafamilia ya marehemu Jaji Zubeir Juma Mzee, wakitafakar jambo wakati wa kupokea mkono wa pole kutoka kwa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi Kijijini kwao, Mbuzini, Wilaya ya Magharibi “A”.(Picha zote na Hassan Issa – OMPR – ZNZ)

No comments:

Post a Comment