Mwanariadha wa Nigeria Lauritta Onye alionyesha mbwe mbwe zisizo za kawaida, kwanza baada ya kushinda dhahabu katika urushaji Tufe ikiwa ndiyo dhahabu wa kwanza kwa Nigeria katika mashindano hayo ya walemavu, na pili ni kuhusu jinsi alivyosherehekea ushindi wake.
Picha zake zimekuwa kwenye mitandao kufuatia ushindi wake katika miongoni mwa wanariadha wafupi. Alirusha tufe umbalia wa mita 8.40 na kuvunja rekodi ya dunia.
Baada ya mashindano kukamilika Onye anaanza kusherehekea
Onye alisherehekea ushindi pamoja na wanariadha wengine akiwemo Rima Abdelli wa Tunisia ambaye alishinda fedha na Lara Baars wa uholanzi ambaye alishinda shaba.

No comments:
Post a Comment