TANGAZO


Wednesday, August 24, 2016

WATUMISHI WIZARA YA HABARI WATAKIWA KUWA WABUNIFU KATIKA UTENDAJI KAZI

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na Watumishi wa Wizara yake wakati wa kikao kazi na watumishi wa Wizara hiyo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Tarehe 23 Agosti 2016. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel akizungumza na Watumishi wa Wizara yake wakati wa kikao kazi na watumishi wa Wizara hiyo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Tarehe 23 Agosti 2016. 
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi. Nuru Millao akiteta jambo na Watumishi wa Wizara yake (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Wizara hiyo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Tarehe 23 Agosti 2016. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Elisante Ole Gabriel. 
Mkurugenzi Msaidizi wa Utawala, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Erast Mushi (kushoto) akitoa ufafanuzi wa mambo yanayohusu Idara yake kwa Watumishi wa Wizara hiyo (hawapo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi wa Wizara hiyo jana katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam Tarehe 23 Agosti 2016.  Wapili kushoto ni Katibu Mkuu Prof. Elisante Ole Gabriel, wapili kulia ni Naibu Katibu Mkuu wizara hiyo Bibi. Nuru Millao na kulia ni Mwenyekiti wa TUGHE Bibi. Magreth Mtaki. 
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bibi. Zawadi Msalla, akijitambulisha kwa watumishi wa wizara hiyo (hawapo pichani), wakati wa kikao kazi na watumishi wa wizara jana katika Uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam Tarehe 23 Agosti 2016. Kulia ni Afisa Michezo Mwandamizi wa Wizara, Bw. Nicolas Bulamile.

Na Genofeva Matemu – WHUSM
Tarehe: 24/08/2016
WATUMISHI Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wametakiwa kuwa wabunifu na kutumia mbinu mbalimbali za kiutendaji kazi ili kuweza kuifanya Wizara kujulikana na kuleta maendeleo katika jamii.

Rai hiyo imetolewa na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel alipokutana na wafanyakazi wa Wizara hiyo jana Jijini Dar es Salaam.

Prof. Gabriel amesema kuwa jamii itathamini kazi za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kama Watumishi wa Wizara watafanya jitihada za makusudi kwa kuwa wabunifu katika utendaji kazi hivvo kuleta tija na heshima kwa Serikali.

“Ni vema kila Mtumishi akajituma katika kukamilisha majukumu ya Wizara yetu kwa kasi na kwa wakati huku tukithamini maslahi ya jamii tunayoitumikia” alisema Prof. Gabriel.

Aidha Prof. Gabriel amewataka Watumishi wa Wizara hiyo kuheshimiana na kuishi kama ndugu kwani muda mwingi hutumia wakiwa ofisini na kuwahaidi kuwa kwa upande wake atahakikisha kuwa watumishi wote wanaishi katika mazingira rafiki katika eneo la kazi.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyakazi wa Serikali Kuu na Afya (TUGHE), Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bibi. Magreti Mtaki amewataka watumishi wa wizara kuacha kungojea fursa zinazopatikana nje ya Wizara bali kutumia fursa zinazopatikana ndani ya Wizara kwani ni rahisi kuzisimamia na kuziendeleza kwa maendeleo ya Taifa letu.

No comments:

Post a Comment