Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Mhe. Jordan Rugimbana kuongea 'live' kuhusu masuala mbalimbali ya mkoa wake.
KATIKA muendelezo wa vipindi vya kuelimisha na kuhamasisha uhamiaji wa serikali kuelekea Makao Makuu Dodoma, TBC imekuwa ikirusha kipindi cha "SAFARI YA DODOMA" ambacho ni cha moja kwa moja (LIVE) kila jumatano saa 3 usiku. Katika kipindi cha leo jumatano tarehe 24 Agosti 2016, tutakuwa na wageni wawili.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, ambaye atatujuza kuhusiana na matarajio ya mkoa wa Dar es Salaam baada ya Wizara za serikali kuondoka jijini. Pia mgeni wa pili ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, mhe. Jordan Rugimbana, ambaye atatueleza ni jinsi gani mkoa wa Dodoma umejipanga kuupokea ujio wa serikali na changamoto zote.
Usikose kutazama kipindi hiki TBC1 saa 3 usiku, na marudio kesho yake Alhamisi tarehe 25 Agosti 2016 saa 2 asubuhi, na Ijumaa tarehe 26 Agosti 2016 saa 12 jioni.
Godfrey Semwaiko
Mratibu wa kipindi.
No comments:
Post a Comment